Friday, May 10, 2013

TFF yamva Dauda, yampa siku saba kujieleza

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtaka Shaffih Dauda mmiliki wa tovuti ya www.shaffihdauda.com, kutoa maelezo kuhusiana na barua ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) aliyoiweka kwenye mtandao wake.

Fifa ambayo ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa TFF baada ya baadhi ya wagombea kuulalamikia na baadaye

kutoa maelekezo kuhusu mchakato huo kwa barua ambayo iliituma kwa Rais wa TFF, Leodegar Lenga ambaye hakutaka barua hiyo ichapishwa katika vyombo vya habari hapa nchini.

Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kuwa katika mkutano wa waandishi wa habari dhidi ya Rais na TFF uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam mara baada ya shirikisho hilo kupokea barua ya Fifa, ambao

Dauda alihudhuria, Tenga alibainisha kuwa barua hiyo hawezi kupewa kila mtu, na kuruhusu waandishi kuisoma kwa bila ya kuondoka nayo.

“Hata hivyo wakati Rais Tenga anazungumza na waandishi wa habari (Mei 2 mwaka huu), nakala ya barua hiyo ya Fifa ilikuwa kwa viongozi wakuu wa TFF pekee, na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pekee.

“Jambo la kushangaza baada ya siku chache barua hiyo
ilionekana imewekwa katika tovuti ya inayomilikiwa na Shafii Dauda,” alisema Wambura.

Alisema kufatia hali hiyo TFF imemtaka Dauda kutoa maelezo ya mahali alipoipata barua hiyo ndani ya siku saba na akishindwa kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Dauda alisema akiwa kama mwandishi wa habari anajukumu la kuandika habari za uchunguzi hivyo baada ya TFF kukataa barua hiyo isichapishwe katika vyombo vya habari ilibidi afanye uchunguzi ili kujua kilichoandikwa ndani yake.

“TFF baada ya kupata barua hiyo walituita kutueleza walichoagizwa na Fifa huku wakikataa barua hiyo

isichapishwe katika vyombo vya habari na mimi ndipo nilipoamua kufanya uchunguzi wangu ili kujua kuna nini
kingine kilichoandikwa ndani ya barua hiyo ambacho TFF hawataki kijulikane,” alisema Dauda.

Alisema pamoja na TFF kumutaka atoe maelezo ya mahali alipoita barua hiyo ndani ya siku saba hato weza kutaja alipoipata kama maadili ya taaluma yake ya Uwandishi wa habari yanavyomtaka pindi anapo andika habari za uchunguzi na hadi anakufa. (Iwapo uongozi huo wa Yanga itatoa kiasi hicho cha fedha basi kila mchezaji atakuwa amevuna shilingi5 milioni.
source; mwananchi



Love to hear what you think!