Tuesday, May 14, 2013

MWIZI KWA KUTUMIA BODABODA AUAWA!

Na Makongoro Oging'
KIJANA mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja anayedaiwa ni mzoefu wa wizi kwa kutumia usafiri wa pikipiki ‘bodaboda’, ameuawa baada ya kumliza mwanamke aliyetambulika kwa jina la Jusmini.
Mwizi wa kutumia usafiri wa Bodaboda akisulubiwa.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Mwenge jijini Dar, saa tatu usiku ambapo inadaiwa mwanamke huyo alikuwa akikatiza mitaa hiyo huku akiwa ameweka mkoba wake kwapani.
Ikadaiwa mwanamke huyo akiwa eneo hilo huku akiamini yuko salama, ilitokea bodaboda kwa nyuma ikiwa imebeba abiria na ghafla alishangaa anakwapuliwa mkoba wake.
“Unajua yule mama alikuwa akitembea kwa kujiamini lakini inavyoonekana wale jamaa ambao ndiyo zao kuwaibia watu walikuwa wamemlia ‘timing’ tangu aliposhuka kwenye daladala.
“Tuliposikia makelele ya mwizi, tulimfuata mama huyo na tulipomuuliza akatuambia ameibiwa mkoba wake huku akituonesha vijana hao ambao muda huo walikuwa wakikimbia,” kilieleza chanzo hicho kilichoshuhudia tukio zima.
...Akiwa hoi baada ya kipondo.
Ikaelezwa kuwa, kufuatia maelezo ya mwanamke huyo, baadhi ya watu wenye hasira kali wengine wakiwa kwenye pikipiki waliamua kuwakimbiza wezi hao ambapo mmoja alishuka na kukimbia kivyake huku mwenye bodaboda akizuiwa kwenye geti kuu ya kutokea magari.
“Alipozuiwa akaona imeshakua soo, akashuka na kuitelekeza pikipiki yake kisha akataka kudandia gari nyingine lakini watu wakafanikiwa kumkamata kwenye mataa ya Mwenge ambapo magari yalisimama, jamaa alishushiwa kichapo hadi akauawa,” kiliendelea kupasha chanzo hicho.
Baada ya kijana huyo kuuawa, polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wake. Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela (pichani)alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema taarifa za kifo cha kijana huyo hazijafika mezani kwake lakini akasema anaendelea kufuatilia.Love to hear what you think!