Saturday, May 18, 2013

DIVA AIFUNGUKIA NDOA YAKE NA PREZZO

Na Hamida Hassan
MTANGAZAJI wa Kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Redio,  Loveness Malinzi ‘Diva’ ameifungukia ndoa yake na staa wa muziki wa Kenya, Jackson  Makini ‘Prezzo’ kuwa haiko mbali kwani hatua waliyofikia ni nzuri.
Loveness Malinzi ‘Diva’ katika pozi na staa wa muziki wa Kenya, Jackson  Makini ‘Prezzo’.
Akipiga stori naGazeti la Ijumaa hivi karibuni Diva alisema uhusiano wake na jamaa huyo hakuna wa kuutibua na anamshangaa msichana anayejitambulisha kwa jina la Boss lady anayedai ameingiliwa.
“Mimi namshangaa huyu dada anayeniandama kwenye mtandao toka aliposikia nipo na Prezzo, kwa kifupi kwa Prezzo nimefika na ndoa muda si mrefu utapita ili tuweze kuishi kama mke na mume” alisema Diva.
Diva alisema kuonyesha kuwa anakubalika hata kwenye familia ya Prezzo, aliongea na dada wa msanii huyo ambaye alimtuliza kwa kumwambia kuwa asisikilize maneno ya watu kwani yeye ndiye wifi yake wa ukweli.
Love to hear what you think!