Sunday, April 7, 2013

MSANII AFA AKIJIDUNGA

Stori: Denis Mtima
MSANII chipukizi wa muziki wa kizazi kipya aliyetambulika kwa jina moja la Rocky mkazi wa Kawe, Dar amefariki dunia baada ya kujidunga madawa ya kulevya.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia tukio hilo na kuomba hifadhi ya jina lake, marehemu anayekadiriwa kuwa na umri wa
Ray C
miaka 23-27, alipatwa na mauti Machi 27, mwaka huu baada kunywa vidonge kumi vya dawa za kulevya aina ya Valium kisha kujidunga sindano tatu za Cocaine.

Langa
Chanzo hicho kilidai, marehemu alikuwa akionywa mara kwa mara na ndugu zake lakini alikuwa akikaidi hali ambayo ilisababisha akamatwe na kuswekwa jela kwa miezi kadhaa kabla ya kuachiwa.
“Marehemu alitoka Segerea juzi Jumatatu (Machi 25) na Jumanne akaanza kutumia tena dawa za kulevya kama kawaida, akajidunga vidonge kumi kwa mpigo.

Aisha Madinda
“Akaweka kete tatu kwenye bomba la sindano tayari kwa kujidunga ndipo alipozidiwa na kupatwa na umauti akiwa bado hajakamilisha zoezi hilo,’’ kilidai chanzo hicho.
Kabla ya marehemu hajazikwa katika makaburi ya Kawe, askari walifika katika eneo hilo ambapo walibainisha kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la vijana kutumia madawa ya kulevya katika eneo hilo.
Lord Eyez
“Vijana wengi hapa Kawe wamejiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya. Tunawashauri hasa hawa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao walitangaza kuacha basi waache kweli maana wakirudia basi kifo kinawaita.

Msafiri Diof
“Historia inaonesha kuna wimbi kubwa la wasanii ambao wamekuwa wakitumia madawa ya kulevya kwa siri kubwa,” alisema afisa mmoja wa polisi aliyeomba hifadhi ya jina kwa kuwa siyo msemaji


Love to hear what you think!