Thursday, March 21, 2013

UKATILI 100%

Na Patrick Mabula, Kahama
HUU ni ukatili kwa 100%! Martha Charles (22), mkazi wa Nyahanga wilayani hapa ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama ameuawa kinyama kwa kuchinjwa shingoni na mume wake,
Marehemu Martha Charles (22) baada ya kuchinjwa shingoni na mume wake, Isack Nzwalile. (29).
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Afande Onesmo Lyanga alisema tukio hilo lilitokea katikati ya wiki iliyopita ambapo pia alimtaja mume anayedaiwa kutekeleza unyama huo kuwa ni Isack Nzwalile (29), mfanyabiashara wa bucha la nyama ya ng’ombe.
 
Isack Nzwalile aliyemchinja mkewe, Martha Charles.
Afande Lyanga alisema mtuhumiwa alimchinja  mkewe wakiwa wamelala chumbani kwenye nyumba ya wazazi wa mwanaume huyo na baada ya kufanya ukatili huo alikimbia.
Jessica Elialinga (19) baada ya kuchinjwa na mpenzi wake, Musa Petro (27).
Habari za uhakika zilizopatikana kutoka katika familia ya marehemu zilisema chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia ambapo mtuhumiwa alianza kwa kumlaumu mama yake mzazi kwa kitendo cha kumtafutia kazi mkewe katika Halmashauri ya Mji wa Kahama wakati yeye alikuwa hataki mkewe afanye kazi.
 
Musa Petro aliyemchinja mpenzi wake Jessica Elialinga.
Habari zilizopatikana eneo la tukio kutoka kwa mmoja wa ndugu anayeishi na familia hiyo, Paul Edward alisema mbali na kuchinjwa shingoni pia marehemu alikatwakatwa sehemu mbalimbali za mwili wake.
 
Marehemu Martha Charles (kulia) enzi za uhai wake akiwa na rafiki yake.
Edward alisema usiku wa tukio akiwa amelala katika moja ya chumba ndani ya nyumba hiyo, alisikia kelele za ugomvi kutoka kwenye chumba cha wanandoa hao hali iliyomfanya apige kelele zilizowafikia majirani ambao walifika kutoa msaada.
Akasema majirani hao sanjari na yeye walimkuta mtuhumiwa ameshamchinja mkewe kwa kisu na kutoweka kusikojulikana.
 
Marehemu Martha Charles akiwa na mumewe, Isack Nzwalile wakifurahia maisha enzi za uhai wake.
Nao majirani waliokwenda kutoa msaada ambao hawakupenda majina yao yatajwe gazetini, walisema walikuta mwili wa Martha ukiwa kitandani huku amekatwa na kitu chenye ncha kali katika eneo lote la shingo, ndipo walipomchukua na kumkimbiza hospitali lakini tayari alikuwa ameshakata roho.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Noel Mkisi alisema baada ya muuaji huyo kutoroka usiku huohuo jitihada za kumsaka zilianza.
Tukio la kuchinjwa kinyama kwa mwanamke huyo limetokea siku chache baada ya hivi karibuni, mchuna ng’ombe Musa Petro (27) naye kumuua kwa kumchinja kwa kisu mpenzi wake, Jessica Elialinga (19).
 
Jessica Elialinga enzi za uhai wake.
Naye Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Maduka ya Nyama Kahama, Faraji Mohamed akiongea na gazeti hili alisema Petro ni mfanyakazi wa Nzwalile katika duka lake la nyama (bucha) ambapo alishangaa kusikia Nzwalile amemchinja mke wake kama alivyofanya mfanyakazi wake, Petro.
Wakati tunakwenda mitamboni habari zilizopatikana kutoka Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kahama na kudhibitishwa na OCD George Simba zilisema mtuhumiwa huyo amekamatwa.



Love to hear what you think!