Saturday, January 12, 2013

MASTAA KIBAO WAHUDHURIA " "EXCLUSIVE LISTENING PARTY" YA WIMBO WA VANESSA MDEE UITWAO "CLOSER"



Jana katika kiota cha Java Lounge kilichopo maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam kulifanyika ‘exlusive’ listening party ya wimbo mpya wa Vanessa Mdee uitwao Closer.

Party hiyo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali waliokuja kumpa shavu mtangazaji huyo wa Choice Fm na MTV Base.

Miongoni mwa maceleb waliohudhuria ni pamoja na Ommy Dimpoz, Jokate Mwegelo, watangazaji wenzie wa Choice FM Thandi Kathembe, Abby Abby Plaatjes na Evance Bukuku, Julio, producer Lucci, watangazaji wa Clouds FM, Adam Mchomvu, Steve B, Dina Marios, DeeAndy na Sade.

Wengine ni Fezza Kessy, Reuben Ndege, Avid, Wakazi na Gosby.

Katika party hiyo Vanessa alielekea upande wa Dj katika Lounge hiyo na kuzungumza mambo kadhaa kabla ya kuucheza wimbo huo. Mdundo wa Closer ulisikika vema kwenye speaker za Java Lounge kiasi cha kuwafanya waalikwa kushindwa kujizuia kushangilia na kuomba urudiwe tena. 

“Attendance imekuwa poa yaani halafu mimi sijaalika mtu personally kwahiyo kutokana na promo tulioifanya Choice FM na Clouds FM watu wamekuja,” alisema Vanessa.

“ So it’s nice kuna watu positive watu wanaosupport movement so am really excited they are here, bado tuko mwanzo, it’s very interactive, najua ni kitu ambacho hakijafanyika Tanzania before so napenda kuwa intimate na fans wangu, those people who are listening to the music, wana support, wanadownload , kujua maoni yao juu ya nyimbo so that why nimefanya hiki kitu.”

Vanessa amesema sababu ya kuachia wimbo wake mwenyewe kipindi hiki haitokani na jinsi watu walivyomkubali kwenye collabo alizofanya bali huo ni mpango uliokuwepo kwa muda mrefu.

“Market ya Tanzania ni kama haitabiriki, so I was a bit sceptical but namshukuru Ommy Dimpoz kwa kunishirikisha kwenye nyimbo yake pamoja na AY. 

Wao wanasimama peke yao lakini ni kama favour wamenipa kamba nicollaborate nao and I am grateful for that forever kwasababu wameniintroduce kwa audience yao.”

“Video ya Closer itakuwepo before March,” alisisitiza Vanessa. 

Asilimia kubwa ya watu waliohudhuria hafla hiyo wamesema Closer ni wimbo mzuri utakaomfikisha mbali mtangazaji huyo.

“Kwakweli I am in love with this track,” alisema Tinashe aka Avid ambaye ni msanii wa R&B. It’s a beautiful song, the quality of production ni nzuri, sikutegemea local production ikawa at this level. Cha pili ni kwamba I think she is grown as an artist.”

“Closer ni wimbo ambao unapeleka Bongo Flava kwenye level nyingine,” alisema Fezza Kessy ambaye ni rafiki wake wa karibu na Vee. “It’s English na Kiswahili mix a bit kwahiyo unakuta wote tunaelewa kama watanzania na international pia wataelewa. It’s nice R&B, the arrangement, the vocals kila kitu you can tell kwamba imefikiriwa na ikawa executed vizuri, it’s a beautiful song.”

Akiuzungumzia wimbo huo naye Ommy Dimpoz amesema, “Siku ya kwanza amenisikilizisha Closer kilikuwa ni kidemo Fulani hivi kifupi ni siku ambayo tunatoka kurekodi Nai Nai kwahiyo I know that song kwamba nikajua kabisa hii single itakuwa kali, kikubwa zaidi nimeona ukubwa wa Vanessa sasa, yeye kama yeye.”

“Vanessa ni msanii mkali sana. Katika wanadada ambao kiukweli wanaimba hapa Tanzania ile ni hazina.”
Tazama picha mbalimbali za za party hiyo hapo chini:
Julio na LeahJulio na Leah
Reuben Ndege na VanessaReuben Ndege na Vanessa
Abby (kushoto), Avid (Kulia) wakiwa na rafikiAbby (kushoto), Avid (Kulia) wakiwa na rafiki
Vanessa akiwa na rafikiVanessa akiwa na rafiki
Reuben na Lucci wakitanianaReuben na Lucci wakitaniana
DSC_2553 (600x402)
Ommy Dimpoz, Jokate na WakaziOmmy Dimpoz, Jokate na Wakazi
Ommy Dimpoz na JokateOmmy Dimpoz na Jokate
DSC_2562 (600x402)
Producer Lucci na ReubenProducer Lucci na Reuben
Throne BoyThrone Boy



Love to hear what you think!