Tuesday, October 9, 2012

Kocha mpya Azam

Kalunde Jamal
UONGOZI wa Azam umeimarisha benchi la ufundi la timu hiyo kwa kumwajili kocha mpya wa makipa kutoka Serbia, Jean Slobodan.

Afisa Habari wa timu hiyo Patrick Kahemela alisema kuwa kocha huyo ni chaguo la Boris Bunjak katika harakati zake za kuhimarisha benchi la ufundi.

Alisema malengo makuu ya kuletwa kwa kocha huyo ni kuboresha benchi la ufundi ambalo linahitaji kuwa na wataalamu wa kila idara ili kukifanya kikosi kiwe makini.

"Hapa Azam ni sawa na Chuo cha Michezo kwa kuwa kuna timu tatu za vijana na wakubwa moja hivyo ni muhimu kuwa na wataalamu wa kutosha na mwalimu alipopendekeza jina la kocha huyu tulimuunga mkono kwa kuwa lengo ni kufanya tuwe na timu imara iliyokamilika kila idara," alisema Kahemela.

Naye Bunjak alisema anaamini hatakuwa na tatizo kwenye upande wa makipa baada ya kupatikana kwa kocha huyo.

"Kikosi changu kipo vizuri uwanjani na nje ya uwanja wachezaji wana furaha na sasa watafurahi na kufanya vizuri zaidi kwa kuwa kwenye benchi la ufundi kumeongezwa nguvu hivyo kila mchezaji ana sehemu ya kutatulia matatizo yake pindi akitatizwa na suala la soka yaani kipa ana mwalimu wake na wachezaji wa ndani wana mwalimu wao nimefarijika sana," alisema.



Love to hear what you think!