Monday, October 15, 2012

KAMA HUKUIPATA HII ANGALIA PICHA ZA UHARIBIFU NA FUJO ZILIZOFANYWA NA WAISLAM BAADA YA KUKOJOLEWA KWA MSAAFU

 Mawe yametoboa vioo vingi
 Katika madhabahu,pameharibiwa

 Mabenchi yamepinduliwa na kuvunjwa
 Mimbari imechomwa na kuharibiwa



 Ofisi ya Kanisa imechomwa moto
 Wachungaji wa kanisa hili wakisubiria taarifa kutoka polisi
 Hawa wanafanya maombi na nimesikia wakiwaombea waislamu mungu awasamehe
 Vifaa vya uimbaji vimechomwa moto
 Washarika wakiwa kanisani kwao asubuhi hii
 Gari la mchungaji pia limeharibiwa kabisa

 Ofisi ya mchungaji na mwinjilisti zimeharibiwa kabisa
Kushoto ni msikiti walipotokea waislamu kabla ya kuvamia kanisa kulia.nyumba hizi za ibada ziko jirani zikitenganishwa na barabara tu





















Waislam wenye itikadi kali wavamia kituo cha police mbagala KIZUIZ NIwakidai wanamuitaji

mshitakiwa wao haliyekamatwa leo asubui kwa kitendo cha kumnyang'anya binti msaafu na kukojolea leo asubui. kwa kitendo hicho kiliwalazimu police kuwatawanya watu kwa kutumia mabom ya machozi kitendo ambacho kime asili mwenendo wa masomo kama tunavyo ona katika picha wanafunzi wakilia.


Hapa baadhi ya waislamu walioamua liwalo naliwe na kuamua kuwatunishia msuli polisi na kusema pigeni mpendavyo hatoki mtu.


Askari wa jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza ghasia wakiwadhibiti vijana waliokuwa wakileta vurugu eneo la mbagala kufuatia kijana mmoja anaesemekana anasoma kidato cha kwanza kukojolea mkojo Quraan na kusababisha hasira kwa waisilamu hassa vijana ambao walitapakaa mitaani na kuanza kuleta vuru.



Vijana waliosambaa mitaani na kuamsha vurugu kubwa kwenye eneo hilo la Mbagala Kizuiani.





Waisilamu waliotoka msikitini kwenye swala ya Ijumaa walikumbana na kimbembe cha kamatakamata hatakama hawakuwemo kwenye sakata hilo, alama ni kanzu na sijda















Barabara zilikua zikiharibiwa kwa moto ulikuwa ukiwashwa na waisilamu hao wenye hasira.



Maji ya kuwasha yalikuwepo ingawa hayakuweza kuzuia vurugu hizo.







Askari na watuhumiwa wakivuka pamoja kwenye mtaro wa maji taka.






Watuhumiwa wavurugu hizo wakipandishwa kwenye gari la polisi.





Baadhi ya vizuizi vilivyowekwa na waislam eneo la Mbagala Kizuiani wakati wa maandamano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo kupinga kitabu kitakatifu cha Koran kufanyiwa dhihaka na mtoto Emmanuel Josephat ambaye aliitemea mate.

Polisi wakiwa katika kuhakikisha hali ya usalama inaimarishwa katika eneo la Mbagala leo

Mmoja wa waandamanaji akiwa amekamatwana askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)


Baadhi ya magari yaliyoharibika katika maandamano ya waislam leo


HAMISI SALUM BABA MZAZI WA KIJANA AMBAYE MSAAFU WAKE ULIFANYIWA DHIHAKA NA EMMANUEL JOSEPHAT NA KUZUA MAANDAMANO MAKUBWA YALIYOFANYWA NA WAAISLAMU JIJINI DAR

VURUGU kubwa zimezuka baada ya mtoto Emanuel Josephat(14)’ kukojolea kitabu cha Quraan cha dini ya kiislam limeingia katika hatua nyingine baada ya waamini wa dini ya kiisilam kukusanyika wakishinikiza kuachiwa kwa mtoto huyo ili wamuue.

Waamini hao wanaokadiriwa kufikia idadi ya 3000 baada ya kutawanywa na Polisi waliingia mitaani na kuchoma kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), Mbagala Zakhem, Kuharibu Kanisa la Anglican,kuvunja vioo katika kanisa la Wasabato, huku kanisa la Tanzania Assembly of God(TAG), Mbagala Kizuiani wakilichoma moto na kuchukua vifaa vya muziki na kuviunguza hadharani.

Vurugu hizo zilizotokea jana jijini Dar es Salaam, majira ya saa 5 asubuhi ambapo waislamu hao walivamia kituo cha polisi Maturubai,Mbagala Kizuiani.

Vurugu hizo ambazo zimesababisha gari za polisi namba T142 AVV,PT 0966 na T 325 BQP,basi la uda na gari la waandishi wa habari kutoka Clouds zikiharibiwa kwa mawe na waandamanaji hao.

Awali waamini hao walikusanyika katika kituo hicho cha polisi wakimtaka mtoto huyo ambaye alikuwa chini ya ulinzi aachiwe na Polisi walipogoma kufanya hivyo ndipo vurugu hizo zilipoanza.

Kikosi cha kutuliza ghasia kilionekana kuzidiwa nguvu na watu hao ambao walikuwa wakiwatawanya kutoka eneo moja wanakimbilia eneo lingine na kuleta madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufunga barabara.

Hatahivyo baada ya viongozi wa dini hiyo kufika wakiwa wameambatana na Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Sheikh wa Taasisi na Jumuiya za Waislamu kukaa kikao na kamanda wa Polisi Wilaya ya Temeke, David Misime, walifikia muafaka wa kuwaita waislamu hao na kuwatuliza lakini hali iliendelea kuwa si shwari kwani baada ya viongozi hao kuona waandamanaji hao wakikamatwa na kupigwa walikuja juu na kutishia kuondoka.

“Ndio nini sasa sisi tupo hapa kwa kuleta suluhu lakini ili waislamu watulie lakini mnawapiga mbele yetu ndio nini sasa



Love to hear what you think!