 
 
MAHAKAMA
 Kuu Kanda ya Tabora, leo inatarajiwa kutoa hukumu katika kesi ya 
kupinga matokeo yaliyompatia ushindi Mbunge wa Igunga, Dk. Peter Kafumu 
(CCM) kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Oktoba mwaka jana.
Shauri
 hilo lilifunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha 
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Kashindye dhidi ya Dk. Kafumu,
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali na msimamizi wa uchaguzi huo, Protace 
Mgayane.
| Joseph Kashinye, Mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA jimbo la Igunga. | 
Shauri hilo lilianza kusikilizwa rasmi Machi 26 mwaka huu chini ya Jaji Mary Nsimbo Shangali.
Akizungumza
 na Tanzania Daima kwa njia ya simu, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya, 
Silvester Kainda, alisema kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora ilipanga 
hukumu hiyo isomwe Agosti 20 mwaka huu, lakini kutokana na tarehe hiyo 
kuangukia Sikukuu ya Idd, hukumu hiyo itasomwa leo.
Wakili
 wa mlalamikaji, Profesa Abdallah Safari, alizungumza na Tanzania Daima 
kwa njia ya simu jana na kusema kuwa zaidi ya malalamiko 13 
waliyawasilisha katika mahakama hiyo.
 
