Kamishna Paul Chagonja 
JESHI la Polisi nchini kuwachulia hatua
  kali kwa watu ambao  watahujumu zoezi  la sensa  ya Watu  na Makazi  
inayotarajiwa  kuanza Agasti 26 mwaka  huu.
Akizungumza na waandishi wa   habari leo 
jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Oparesheni na Mafunzo wa  Jeshi la 
Polisi, Kamishna Paul Chagonja  alisema jeshi  limejipanga   katika  
kuhakikisha  zoezi la sensa linafanyika  katika  hali  utulivu  
pasipokuwepo na uvunjifu wa amani wa kutaka kuhujumu zoezi hilo.
Chagonja alisema  kuwa watu ambao watafanya
  uhalifu ikiwemo kuchana karatasi za makarani wa sensa watachuliwa   
hatua  kwa  kuwafikisha  mahakamani kutokana  na sheria  ya sensa.
Alisema kuwa kususia  sensa ni kosa ambapo 
 aliwataka wenye malalamiko  kutekeleza zoezi  katika  hali  usalama  na
   baadaye  baada  ya  kazi  hiyo  kukamilika  ndio wafuatilie  madai 
yao.
“Jeshi halitaweza kuwaacha watu ambao  
wanataka  kuhujumu zoezi la sensa  ambalo  liko kisheria kwa  madai  yao
  wanatumia  taasisi  katika  kushawishi wananchi wasijitokeze katika   
zoezi ambalo  watendaji wetu  wametekeleza hadi kufikia  hapo”.alisema  
Chagonja.
Kwa Upande wa Mkurugenzi  wa Makosa  ya  
Jinai Robert Manumba alisema kuwa  tayari  jeshi la polisi   
linawashikilia watu  kutokana  na  kutaka kuhujumu zoezi  hilo.
Alisema  bado wanaendelea  kufuatilia kwa  
karibu juu  ya  watu ambao wanashawishi wananchi kugoma  katika   
kuhesabiwa  kwa  sababu zao ambazo  haziko  kisheria.
Manumba
  aliwataka  wananchi kushirikiana kwa  kutoa  taarifa za watu ambao  
wanaopita kwa kubandika  sitika katika  nyumba juu  ya  kugomea sensa.
CHANZO; http://francisdande.blogspot.com
 
