Friday, July 13, 2012

WOLPER, WEMA WAPONGEZWA


Wema na Wolper wakiwa katika pozi baada ya mpambano wao.
Na Hamida Hassan
MASTAA wa filamu Bongo, Jackline Wolper na Wema Sepetu wamepongezwa na wadau kwa uamuzi waliochukua wa kumaliza bifu lao kwa kuchangia mfuko wa elimu Tanzania.
Wolper na Wema, mwishoni mwa wiki iliyopita walipanda ulingoni ndani ya Uwanja wa Taifa kupigana katika Tamasha la Matumaini ambapo sehemu ya fedha iliyopatikana ilikuwa ni kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wasichana nchini.
Wakizungumza na Ijumaa mara baada ya tamasha hilo, baadhi ya wadau wa filamu walisema walichokifanya mastaa hao ni kitu cha busara kwani wamechangia elimu lakini pia wametumia pambano hilo kumaliza tofauti zao.
“Wameonesha kuwa na busara sana kupatana mbele ya umati wa watu kama vile lakini pia wamechangia katika suala la elimu nchini, wanastahili pongezi,” alisema Said Juma wa Mbagala jijini Dar.
Naye mama Masoud wa Sinza alisema: “Nimefurahi kuwaona ulingoni kisha wakamaliza tofauti zao, unajua wote ni wasanii wakali kwa hiyo kitendo cha kufuta bifu lao kitawafanya siku moja washirikiane kutoa filamu ambayo naamini itakuwa kali.”



Love to hear what you think!