Sunday, July 8, 2012

THEA AJIFUNGUA MTOTO SIYO RIZIKI


Na Gladness Mallya
MSANII mwenye heshima kunako tasnia ya filamu za Bongo, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ (pichani) amejifungua lakini mtoto wake akiwa amefariki dunia.
Chanzo chetu makini kilichoomba hifadhi ya jina lake kilieleza kuwa, Thea alijifungua mtoto wa kike kwa njia ya kawaida usiku wa kuamkia Jumanne iliyopita katika Hospitali ya Marie Stopes lakini akawa siyo riziki.
“Unajua familia yao haikutaka mapaparazi wajue kuwa Thea yupo hospitali kwa ajili ya kujifungua kwa sababu hawapendi magazeti hivyo hapa nimefanya kuwaambia tu msinitaje jamani,” kilisema chanzo hicho.
Aidha, chanzo hicho kiliongeza kuwa mwili wa kichanga hicho ulizikwa katika Makaburi ya Mwananyamala jijini Dar juzi Jumanne asubuhi.
Jitihada za kuwapata Thea au mumewe Mike Sangu ili kuzungumzia ishu hiyo hazikuzaa matunda hadi tunakwenda mtamboni.Love to hear what you think!