Thursday, July 19, 2012

STELA WA VENGU ANASWA AKIMSALITI



Stela Mbuge akiwa na  Juma Chikoka ‘Chopa’.
Na Shakoor Jongo
WAKATI staa wa vichekesho wa Kundi la Orijino Komedi, Joseph Shamba ‘Vengu’ akiwa bado hajapata nguvu ya kuingia mitaani, mchumba wake Miss Kinondoni 2011/12, Stela Mbuge ‘Stela wa Vengu’ amenaswa akiwa na mwigizaji wa Bongo Movies, Juma Chikoka ‘Chopa’ na kuzua maswali tata.
Tukio hilo la ‘maselebreti’ hao lilijiri hivi karibuni ndani ya Ukumbi wa New Maisha Club Masaki jijini Dar ambapo kulikuwa na shindano la kumtafuta Miss Vyuo Vikuu 2012.
Chopa na Stela walikuwa wakiambatana pamoja katika ukumbi huo na walipoona wanapigwa picha walijaribu kuficha nyuso zao.
“Dah bro hizo picha siyo nzuri utaharibu hali ya hewa zikija kuonekana,” alisema Chopa baada ya kumuona paparazi wetu akiwafotoa.
Paparazi wetu alipomfuata Stela na kumuuliza kuhusiana na kugandana na Chopa kwa kipindi kirefu tangu alipoingia ukumbini humo alibaki akijiumauma tu bila ya kutoa jibu sahihi.
“Chopa si ameshakwambia hali halisi kuhusiana na hizo picha, sasa unaendelea kuniuliza maswali ya nini? Cha kufanya ni kuzifuta kwani utakuwa umeamua jambo la maana sana,” alisema Stela.



Love to hear what you think!