Monday, July 16, 2012

KANISA LAKANUSHA KAULI YA POLISI KUHUSU ALIYEMTEKA DOKTA ULIMBOKA!


Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Kawe jijini Dar Es Salaam kupitia mchungaji wake Ndugu Joseph limekanusha kauli iliyotolewa siku chache na jeshi la polisi nchini iliyokuwa ikidai kuwa mtuhumiwa Joshua anayetuhumiwa na utekaji wa Dokta Ulimboka alikamatwa kanisani hapo akiwa amekwenda kutubu kosa la tukio hilo. Akizungumza kupitia ITV mchungaji huyo alisema kauli hiyo si ya kweli kwani mtuhumiwa huyo hakukamatwa akiwa anatubu makosa
hayo bali alikuwa amekuja kanisani hapo kumtafuta mchungaji kiongozi wa kanisa hilo na hakuweza kufanikiwa kuonana naye na ndipo polisi walipokuja kumkamata muda mfupi baadae huku akidai ya kuwa wao hawamtambui mtu huyo na wala kanisa halitoagi siri za waumini wake wanaokuja kutubu hivyo si kweli wao walitoa taarifa ya kuwa mtu huyo yupo kanisani hapo kwa ajili ya kutubu, Pia mchungaji huyo alisisitiza iundwe tume huru ya kuchunguza tukio hilo!


Love to hear what you think!