Thursday, July 19, 2012

IDADI YA WALIOFARIKI DUNIA KWENYE AJALI YA BOTI MPAKA SASA


.
Inawezekana taarifa za ajali ya boti ya Seagul iliyotokea leo mchana Zanzibar ukawa umezisikia au kuzisoma sehemu mbalimbali lakini kauli hii ya Waziri wa mambo ya ndani imetoka muda mfupi uliopita. 
Waziri Emmanuel Nchimbi akiongea na TBC1 amesema “vikosi vya uokoaji vinaongozwa na mkuu wa jeshi la polisi Inspekta Jenerali Said Mwema vinaendelea na uokoaji”
Kuhusu watu waliopoteza maisha au kuokolewa Waziri Nchimbi amesema “Katika abiria wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 250 waliokua wamebebwa na boti hiyo, wameokolewa 124 wakiwa hai na waliothibitishwa na jeshi la polisi kufariki dunia ni saba tu, juhudi kubwa za uokoaji zinaendelea”


Love to hear what you think!