Tuesday, July 24, 2012

Dar Express, Simba Mtoto yagongana uso kwa uso

Basi la Dar Express lililokuwa linatoka Arusha na basi la Simba Mtoto lililokuwa linaenda Tanga yamegongana uso kwa uso maeneo ya Wami. Mwanahabari wa "Globu ya Jamii" aliyekuwa eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali kutokea anasema hadi anaondoka mahali hapo hakuna maafa ya watu kupoteza uhai yaliyoropotiwa ila, watu kadhaa wamejeruhiwa na kuna mtu mmoja amebanwa katikati ya mabasi ambayo kisa cha kugongana kwake bado hakijafahamika.

Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya Chalinze.
Picture
Abiria wa wakishushwa kupitia madirishani
Picture
Picture
Abiria wakijaribu kumwokoa mwenzao aliyenaswa
                      Picture


Love to hear what you think!