Wednesday, July 25, 2012

BIIBI LULU AMWAGA CHOZI KISUTU

 
Lulu akiwapungia mkono bibi yake, ndugu na jamaa.
 
Ndugu na jamaa wakimpungia mkono Lulu.
Na Richard Bukos
HUKU kesi ya kushukiwa kuhusika  na mauaji ya marehemu Steven Kanumba ikiendelea kumkabili nyota wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, bibi yake na msanii huyo alitinga kortini kusikiliza kesi ya mjukuu wake.
Bibi huyo ambaye alitajwa kwa jina moja la Elizabeth, ilielezwa ni mama mzazi wa mama wa msanii huyo Lucresia Karugila, alitinga katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, juzi, Jumatatu, jijini Dar es Salaam akiwa ameongozana na mwanaye (mama’ke Lulu) na ndugu wengine.
Shauri hilo lilifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa kupelekwa Mahakama ya Rufaa, kama mawakili upande wa serikali walivyoomba katika kesi hiyo.
“Huyu ni bibi yake Lulu, amekuja kutokea kijijini Bukoba. Ni mama yangu mzazi. Ameguswa na jambo hili na ameona ni vyema aje kumuona mjukuu wake,” alisema mama Lulu.
Kesi hiyo imehairishwa na Msajili wa Mahakama hiyo, Amiri Msumi, mpaka Agosti 20 mwaka huu kwa vile jaji aliyetakiwa kusikiliza kesi hiyo Twalib Fauz hakufika mahakamani hapo kwa kile kilichoelezwa alikuwa na dharura. Lulu alirudishwa mahabusu katika Gereza la Segerea kusubiri tarehe hiyo.




Love to hear what you think!