Kiongozi
wa kanisa hili (White Tail Chapel), Pastor Allen Parker amesema kuwa
ameamua kuwaruhusu waumini wa kanisa lake kuingia kanisani bila nguo ili
kuweka usawa kati yao mbali na mavazi na vitu vya kidunia.
Pastor Allen pia amekuwa akisimamia
mafundisho yake haya kwa kuzingatia hadithi za Maandiko Zikiwepo za Adam
na Hawa kukaa uchi katika bustani ya Eden bila aibu, Kuzaliwa bila kuwa
na nguo pamoja na mambo mengine yanayofanana na hayo.

Hata
hivyo, Swala la kuingia katika Kanisa hili bila nguo limefanywa kuwa la
hiyari hivyo kwa wale wanaojisikia kuingia wakiwa wamevaa nguo
huendelea kufanya hivyo kama kawaida.