Mastaa wa filamu, Manaiki Sanga na Wema Sepetu wanadaiwa kuwa wapenzi.
Habari ni kuwa wasanii hao walianza kama marafiki wa kawaida na baadaye
Manaiki kurusha kete yake kwa Wema Sepetu...
Kwasasa wawili hao inasemekana wapo karibu sana kiasi cha kuzua minong'ono kwa wafuatiliaji wa habari za mastaa nchini.
"Manaiki Sanga amemnasa Wema katika himaya yake, wapo karibu sana siku
hizi hata marafiki zao(wa Wema na Manaiki) wanajua kuwa wanatoka pamoja,
si wajua Manaiki ni playboy na akiamua kumpata girl yeyote yule
hashindwi??" kilisema chanzo hicho ambacho pia ni msanii wa filamu
nchini
Naye Manaiki Sanga ambaye
siku za hivi karibuni alikumbwa na skendo ya kutembea na kupiga picha
chafu na wasichana kibao alipotafutwa na kuulizwa kuhusu kuwa katika
mapenzi na Wema Sepetu alijibu kwa ufupi kwa kusema "ni wazushi".
Manaiki alipoulizwa tena kama ukaribu wake na Wema ni wa kikazi au
wanashuti filamu pamoja, alijibu kwa kusema: "Nililala siku nne kwake
wakajua demu wangu!!!"
Alipododoswa zaidi kwanini alale nyumbani kwa Wema wakati Wema yupo na
Diamond kwasasa kama wapenzi alijibu "Diamond alikuwa anafungiwa ndani ,
alikuwepo"