Nyumba
ya familia moja huko mtaa wa ugombolwa Kata ya Segerea ikiwa
inateketea kwa moto usiku huu mara baada ya Baba wa familia hiyo kuhisi
kuwa mke ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mmoja na kuamua
kuichoma moto nyumba hiyo sababu ya wivu wa mapenzi.
Nyumba ikiendelea kuteketea kwa moto mkali
Kwa moto huu hakuna kilichoweza kuokolewa mpaka sasa
Baadhi ya Wakazi wa Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea Wilaya ya Ilala Jijini Dar wakishuhudia nyumba hiyo ikiteketea kwa moto.
Segerea, Dar Es Salaam, Nyumba moja iliyopo Mtaa Ugombolwa Kata ya
segerea Jijini Dar imeteketea kwa moto mara baada ya baba wa familia
ya nyumba hiyo kuhisi kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume
mwingine.
Hali hiyo imetokea usiku huu majira ya Saa tano Kasoro usiku Jana Jumatatu katika Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea, Wilaya ya Ilala Jijini Dar Es Salaam ambapo inasemekana baba wa familia hiyo alichukua uamuzi huo mara baada ya kusikia kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine nje na mara baada ya kutokuelewa kwao ndipo alipochukua uamuzi huo wa kuitia moto nyumba hiyo.

Mmoja wa shuhuda alisikika akisema kuwa "Hawa
Wachaga wana matatizo sana Ebu Ona Sasa mwanaume Mzima Anateketeza
Nyumba yake aliyoijenga kwa mamilioni ya Shilingi kisa Mkewe anatembea
nje ya ndoa Sasa ona watoto wake wataishi wapi?..watu wengine ni
wajinga sana Kama mwanamke anatembea nje ya ndoa si umpe talaka tu" alisikika akiongea Shuhuda huyo.
Mpaka Mtandao huu unaondoka eneo la tukio nyumba hiyo ilikuwa bado
ikiteketea kwa moto na hakuna dalili zozote zile zilizokuwa
zikichukuliwa kwaajili ya kupambana na moto huo huku ikiwa
haijafahamika kama wakati nyumba hiyo ikitiwa kiberiti familia ya huyo
baba ilikuwepo ndani ya nyumba au laah huku ikikadiriwa kuwa mali zote
zilizomo ndani ya nyumba hiyo zimeteketea kwa moto kwani mpaka
tunaondoka hakuna kikosi cha zimamoto kilichofik eneo la tukio wala
majirani hawakuonyesha dalili zozote zile za kuuzima mot huo.
Mpaka tunaondoka eneo la tukio hakuna taarifa yoyote ile ya majeruhi wala watu kupoteza maisha katika ajali hiyo ya moto