Mwigizaji wa kike anayetesa katika tasnia ya filamu Bongo Diana Rose kimaro ‘Diana’ amedai kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yoyote na wala hafikirii kuwa na Boyfriend kwani yeye bado ni mwanafunzi na akili yake yote ipo katika masomo .
Wakati ukifika akiwa na maisha yake atachagua ni mwanaume yupi anastahili kuwa naye kwa maisha yake rasmi lakini si sasa.
“Sijui kabisa mambo hayo na sijawahi kufanya upuuzi huo, ninaheshimu sana familia yangu baba yangu ni mkali sana hataki ujinga. Kwa hiyo si rahisi kudili na wanaume, mimi ni bikira , natoa nafasi kwa masomo kwanza sitaki kujichanganya na kuwa kituko mjini,” anasema Diana.