Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba Padre Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki Zanzibar ameuawa kikatili kwa kupigwa risasi tatu kichwani leo asubuhi. Padre Evarist alikuwa anakwenda kuongoza ibada takatifu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Teresia lililopo Mtoni Zanzibar. Marehemu alikuwa anakaribia kanisani majira ya saa 1.30 asubuhi na ameuawa mbele ya waumini wa kanisa lake. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN