STAA wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ anadaiwa kuishi maisha ya kujificha machoni mwa watu wengi hasa wasanii wenzake, Ijumaa limeelezwa.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya RJ aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kwa sasa bosi wake huyo hataki kabisa kukutana na baadhi ya rafiki zake wakiwemo wasanii kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kutokana na aibu ya kupigana na msanii mwenzake, Chuchu Hans wakigombea mwanaume.
“Kwa sasa Johari hataki kabisa kuonana na watu wake wa karibu, hata mtaani amekuwa haonekani mara kwa mara, anawakwepa hata wasanii wenzake, hii ni kutokana na lile sakata lake na Chuchu,” alisema mtoa habari huyo.
Ijumaa lilimpata Johari na alipoulizwa juu ya sababu ya kujifungia ndani alisema: “Niko nyumbani, sitaki kutembea sana kwani niko na likizo fupi, halafu hata hili sakata langu na Chuchu bado halijapoa.”