Sunday, November 18, 2012

MWENYEKITI WA CCM RAIS KIKWETE AREJEA ALAKIWA KWA SHANGWE


Rais Jakaya Kikwete akipokewa kwa shangwe na wafanyakazi wa Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kurejea akitokea Arusha alikokuwa katika ziara ya siku mbili ya kikazi na kabla ya hapo alikuwa Dodoma ambako alichaguliwa tena kuongoza CCM kwa miaka mingine mitano.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bw Madabida na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Said Mecky Sadik.
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bw Madabida na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Mhe. Philip Mangula na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Said Mecky Sadik.
(PICHA NA IKULU)




Love to hear what you think!