Ambwene Yessaya 'A.Y'.
VIDEO ya wimbo
I Don’t Want To Be Alone imempatia tuzo
msanii mahiri wa Bongo Fleva nchini, Ambwene Yessaya 'A.Y'. AY
amefanikiwa kunyakua tuzo katika kipengele cha Most Gifted East African
Video of the Year kwenye tuzo za Channel O Music Video Awards 2012
zilizofanyika Walter Sisulu Square mjini Kliptown, Soweto nchini ya
Afrika Kusini.
Wasanii waliokuwa wanawania tuzo hiyo aliyojinyakulia AY ni:
Keko Feat. Madtraxx – Make You Dance
Camp Mulla – Party Don’t Stop
K’Naan Feat. Nas – Nothing To lose
Navio – One & Only