Amber Rose ambae ni girlfriend wa Rapper Wiz Khalifa ameandika tweet kwa followers wake million 1.4 iliyotaja jinsia ya mtoto wao wanaemtarajia. lakini katika tweet hiyo anaonesha kama hakuwa na plan ya kutaja jinsia ya mtoto huyo ila ni kama ameitaja accidentally,wanatarajia mtoto wa kiume.
Lakini hii inawezekana aliamua tu kwa sababu ameandika katika tweet moja hiyo hiyo message inayotaja jinsia ya mtoto wao mtarajiwa na hapo hapo anashtuka kama kataja bila kujua.
Tweet yake ya jumapili ilikuwa inasomeka “My friend Maria bought our Lil Boy this Slash onesie….Oops did I say Lil Boy???
Hivi karibuni pia Amber Rose alipokuwa anazungumzia mipango yao ya kumpokea mtoto wao katika maisha yao alisema wanapanga kuoana kwanza kabla hajajifungua mtoto.
“Nah, hakuna tarehe iliyopangwa bado. Lakini tunaweza kupata license na kufunga ndoa kabla mtoto hajazaliwa, na tutafanya sherehe baadae kwa sababu italeta maana kwa mtoto kuzaliwa katika wedding na zaidi ya kuwa katika hii hali ya ujauzito tu. Watu wengine wanaharakisha na kufanya. Lakini njia zote zinawezekana” alisema Amber Rose