Na Juventus Juvenary wa Mjengwablog, Kibondo
Watu watatu wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma wakitibiwa majeraha ya Risasi
Tukio
hilo linafuatia watu wanaosadikiwa kuwa majambazi waliovamia Gari
walilokuwa wakisafiria na kulishambulia kwa risasi zilizowajeruhi sehemu mbali mbali za miili yao
Waliojeruhiwa
ni Josephat Maimu miaka 31, Shukuru Benet 25 na Noel Godfrey 21 ambao
walikuwa Safarini kutoka Kibondo-Kigoma kuelekea Kahama-Shinyanga katika
shughuli zao za kawaida.