Maelezo ya Dogo Janja
yanaSEMA kwamba juzi (September 2) walivyokua Club Maisha aliperform
akiwa na furaha kutokana na mashabiki zake waliojitokeza na alipomaliza
kuperform alishuka kwenye stage akiwa na furaha baada ya kufanya vizuri
lakini hiyo furaha ilikatishwa baada ya kwenda juu sehemu ya V.I.P
Janja anasema alipopanda V.I.P
kumsalimia Producer Maneck alimjibu kwa dharau na kumwambia haongei na
Masnich hivyo Dogo Janja akaondoka lakini muda mfupi baadae alirudi na
kukuta Tunda Man yuko karibu na alipokaa Maneck, Janja pamoja na Tunda
walimsogelea producer huyo ambae alianza kumtukana matusi mazito Dogo
Janja.
Baada ya hapo ilibidi Dogo
Janja kushuka chini na kwenda kumchukua Ustaz Juma ambae ndio boss wa
kundi alilopo sasa Dogo Janja la Watanashati, walipofika alipo Maneck..
alianza kuiponda single mpya ya Dogo Janja aliyorekodi na producer Marco
Chali kwa kusema wimbo huo ambao mwanzo ulikua urekodiwe kwa Maneck ni
wa kawaida sana.
Kwenye line nyingine namkariri
Dogo Janja akisema “nikawa nimepanic sana sasa leo nakuja kupokea simu
eti Tunda man nae anasema nifute chorus ya ‘Anajua’ kwenye wimbo wangu,
Bro ule wimbo nimeurekodi nikiwa Tip Top na nimeifanyia show nyingi sana
Tanzania ambazo zimewaingizia hela nyingi sana, hawana ubinadamu yani
wanaponiambia mimi nifute chorus, Tunda kawafanyia watoto wangapi
chorus? Shetta, Pasha lakini mbona hamwaambii Pasha afute au labda
sababu mi mdogo, hili swala nawaachia watanzania kwa sababu ile ni haki
yangu, nilimshirikisha Tunda.. ule wimbo sio wa Tunda siwezi kufuta
chorus”
Baada ya hayo maelezo ya Dogo
Janja, Producer Maneck amezungumza exclusive na millardayo.com na
namkariri akisema “Dogo Janja alikuja akanisalimia nikamwambia ebwana
eeeh kaa mbali na mimi sihitaji kuongea na wewe kwa sababu unatabia za
kisnich sana, kuna vitu flani alivifanya siku kadhaa zimepita na
sikupendezwa navyo.. tuliandaa show ya Tunda Man pale Maisha Club
tukamwambia na akakubali kufanya na tukatangaza kwamba atakuepo sasa
mwisho wa siku akabroadcast msg kwenye BBM alafu sisi hakututumia ile
msg ila akabroadcast kwa watu kwamba hao ni matapeli, hapohapo nachat
nae namuuliza mbona umezingua anasema mi naona aibu sijui hata sura
yangu sijui nitaiweka wapi kwa bwana Captain, huku anasema hivi huku
anafanya hivi”
Tunda Man nae ametoa sababu za
kumwambia Dogo Janja afute sauti yake kwenye kolabo waliyofanya ya
‘Anajua’ na nina mkariri akisema ” sikuzungumza kwa ubaya, nimezungumza
kwa nia nzuri tu.. kwenye chorus inasema niko na Captain Tunda man alafu
mimi siko pale mashabiki wanakua kama hawakuelewi vizuri, kuna mistari
mingine inasema narun city nikiwa na JCB, narun Dar City nikiwa na T.I.P
sasa ujue kwenye show kuimba vitu kama hivyo wakati hayupo na Tip Top
vinakua havileti maana, ni kama maoni tu nimemuomba aimbie beat kwa
sababu anaweza kurekebisha ile mistari, mfano kusema narun city nikiwa
na Watanashati, kwenye show ndio abadilishe lakini kwenye audio ni sawa
ikibaki na vionjo vya mwanzo”