Msemaji wa Polisi Mohamed Mpinga ameiambia millardayo.com kwamba Jahazi lilikua linatokea Kusini Pemba kwenda Nungwi kaskazini Unguja ambapo mtoto wa miaka mitano Isaka Hamis alipoteza maisha.
Polisi mkoa wa Kusini Pemba wamesema chanzo cha ajali ni ujazaji wa mizigo uliopitiliza kwani Jahazi hilo lilibeba magunia kumi ya Muhogo, mikungu 10 ya ndizi pamoja na mizigo mingine ya kuni.
Watu sita walinusurika kifo akiwemo mama mwenye mtoto wa miaka miwili, vyombo hivi vya uvuvi vimekua vikitumika kusafirisha abiria na mizigo kimakosa wakati pia havitakiwi kusafiri umbali mrefu.
Source milard ayo