Thursday, July 26, 2012

MISS ILALA No 3 AMTOSA MUMEWE MAHABUSU


Na Waandishi Wetu
Mwanamitindo Jacqueline Patrick ambaye pia ni Miss Ilala no.3, 2005 anadaiwa kumtelekeza mumewe Abdullatif Fundikira aliyepo mahabusu katika Gereza la Segerea, jijini Dar es Salaam kwa madai ya kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Akizungumza na Mwandishi, rafiki wa karibu na mwanamitindo huyo alisema kuwa wenzake wanamshangaa Jack kwa kitendo cha kumtosa mumewe wakati anafahamu yupo katika matatizo makubwa.
“Kiukweli anachofanya Jack si uungwana kabisa, we fikiria tangu mumewe akamatwe (Mei mwaka huu), hajawahi kwenda mahabusu kumtembelea au hata siku ya mahakamani kuhudhuria kusikiliza kesi yake inavyoendelea, yeye na starehe, starehe na yeye,” alisema shostito huyo akiomba kuhifadhiwa kwa jina lake.
Akiendelea kuzungumza, rafiki huyo alisema kuwa kitu kingine ambacho anaamini kuwa ndoa ya Jack ni ndoano ni kitendo cha kuondoka nyumbani kwake na kutimkia nje ya nchi bila mumewe kuwa na taarifa.
“Yaani huyu mwanamke ni wa ajabu sana, hivi ninavyokwambia yupo nje ya nchi huku mumewe akiwa anateseka mahabusu, mbaya zaidi mume hajui,” alisema.
Baada ya kusikia kauli hiyo, Amani lilianza kumsaka Jack kupitia simu yake ya mkononi ambapo muda wote ilionekana haipo hewani lakini kupitia udodosi wa paparazi wetu, lilimnasa staa huyo juu kwa juu kupitia mtandao wa What’s Up ambapo mahojiano yalikuwa hivi:
Shakoor: Jack ningependa kufahamu upo wapi kwa sasa maana nakutafuta kwenye simu yako ya mkononi sikupati?
Jack: Shida yako nini? Sihitaji stori wala promo ya aina yoyote kutoka kwenu.
Shakoor: Mbona umefika mbali? Hata ninachotaka kukwambia hujakisikia unaanza kuwa mkali.
Jack: Hapa hatuchezi drama hicho ndicho ninachoongea, nipo bize na mambo yangu, naomba niache.
Hata hivyo, Jumatatu iliyopita, paparazi wetu mmoja alifunga safari hadi nyumbani kwa nyota huyo, Mbezi, Dar es Salaam ambapo watu waliokutwa ndani walisema Jack amesafiri kwenda ughaibuni bila kutaja jina la nchi aliyoenda.
Mtu wa karibu na Jack alipopatikana na kuulizwa alipo mwanandoa huyo, aliweka wazi kuwa yupo nchini Finland lakini hakusema amefuata nini huko.
“Mimi ninavyojua Jack yuko Finland, sasa lini atarudi au amefuata nini huko, sijui,” alisema.
Imeandikwa na: Shakoor Jongo na Musa Mateja.




Love to hear what you think!