Thursday, July 26, 2012

Mkwere afichua utamu wa ndoa


Hemed Maliyaga ‘Mkwere’ na mkewe Fatma Abadallah siku ya ndoa yao.
Na Gladness Mallya
MCHEKESHAJI wa Kundi la Kashikashi linalorusha michezo yake kupitia Kipindi cha Mizengwe cha ITV, Hemed Maliyaga ‘Mkwere’ ameweka wazi utamu anaouona kwenye ndoa hivi sasa.
Akichonga na Motomoto Newz, Mkwere ambaye alifunga ndoa mwaka jana na Fatma Abadallah na wamepata mtoto mmoja, alisema anaifurahia ndoa yake kiasi kwamba anajilaumu ni kwa nini hakufanya hivyo mapema.
“Yaani ndoa ni tamu jamani, nafurahia mazuri mengi ninayofanyiwa na mke wangu, hata uzito wa mwili wangu umeongezeka, nawaomba wale ‘mabachela’ waoe sasa ili waone raha iliyomo ndani ya ndoa,” alisema Mkwere.




Love to hear what you think!