Thursday, July 19, 2012

BAHARI YAGEUKA KUWA NYEKUNDU KUTOKANA NA DAMU NYINGI ZILIZOMWAGIKA


Bahari ya kisiwa cha FAROE kila mwaka ifikapo tarehe 22 mwezi wa 11 hubadilika na kua nyekundu kutokana na utamaduni wa wakazi wa kisiwa hicho wa wa kuadhimisha siku ya kitaifa ya uwindaji wa NYANGUMI.Sikukuu hiyo ya kitamaduni imepewa jina la GRINDADRAP.Uwindaji huo wa NYANGUMI si kwa ajili ya malengo ya kibiashara kwa sababu nyama za nyangumi hao hugawiwa kwa wananchi wote wa kisiwa hicho.Wavuvi hao huwaburuza NYANGUMI hao hadi pembezoni mwa bahari na kuwakatakata mapande ya nyama na kuacha damu ikitiririka kuelekea BAHRINI na kusababisha BAHARI hiyo kuwa na rangi nyukundu.



Love to hear what you think!