Wednesday, June 3, 2015

Ajinyonga mtini kwa Shati lake.....Kabla ya Kujinyonga Aliwafuata Polisi na Kutaka Awekwe Mahabusu


Mkazi wa Ilembo wilayani Mpanda , Petro Magawe (40) amejinyonga kwa kujitundika mtini akitumia shati lake.

Mtu huyo alijinyonga hadi kufa saa 2 asubuhi juzi karibu na Ofisi ya Misitu iliyopo Mtaa wa Majengo A mjini Mpanda.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari alisema Mei 30 , mwaka huu, Magawe alifika Kituo Kikuu cha Polisi Wilaya ya Mpanda mjini Mpanda, akieleza kuwa alikuwa akihitaji kuwekwa mahabusu .
 
“Badala ya kukubali ombi lake la kuwekwa mahabusu alipata msaada kwa kupewa Fomu ya Polisi namba 3 ( PF 3) ili akatibiwe hospitalini baada ya kuonekana kuwa alikuwa amechanganyikiwa kiakili,” alisema Kamanda.
 
Alisema “Siku iliyofuata asubuhi mtu huyo alikutwa amejinyonga kwa kutumia shati lake mwenyewe.” Alisema polisi inaendelea na uchunguzi wa tukio hiloLove to hear what you think!