Tuesday, February 26, 2013

RIHANNA NA CHRIS BROWN WARIDHIA KUFUNGA NDOA JULY MWAKA HUU


Jarida maarufu (Star Magazine) limeripoti kwamba mastaa wa muziki Chris Brown na Rihanna wanampango wa kufunga ndoa mwishoni mwa July 2013 nyumbani kwa kina Rihanna huko Barbados.
 
Jarida hili limeendelea kutiririka kwamba kwenye ndoa hiyo wamepanga kusherehekea na watu mbalimbali wakiwemo wanaoamini kwamba Chris Brown amebadilika kitabia.
 
Ni harusi ambayo watu wote walioalikwa watakua wamesimama na wahudumu watakuepo kumfata kila mtu alipo, pia wale wachoraji wa tattoo watakuepo pia.

Tuesday, February 19, 2013

PICHA ZA KANISA LILILOCHOMWA MOTO LEO HUKO ZANZIBAR





MAUAJI YA PADRI ZANZIBAR NYUMA YA PAZIA

Na Haruni Sanchawa
MAUAJI ya Padri wa Kanisa Katoliki Zanzibar, Evarist Mushi yaliyotokea juzi (Jumapili) wakati akiingia kanisani kuendesha ibada ya asubuhi, yamezua utata na inadaiwa kuna mambo mengi yaliyojificha nyuma ya pazia.
Akina mama wakilia kwa uchungu kuomboleza kifo cha ghafla cha kupigwa risasi Padri Evarist Mushi kilichotokea juzi asubuhi.
Mauaji hayo yalifanyika kimafia katika Kanisa Katoliki, Kigangwe cha Mtoni saa 12:45 asubuhi wakati akijiandaa kwenda kuongoza ibada kanisani humo.
Kwa mujibu wa ofisa mmoja wa polisi, katika eneo la tukio walifanikiwa kukuta maganda mawili ya risasi na hakukuwa na wizi wowote uliofanyika baada ya padri huyo kupigwa risasi mbili kichwani.
Waumini wa Kanisa Katoliki Zanzibar na wananchi wa mjini Zanzibar wakikusanyika kwenye hospitali kuu ya Mnazimmoja mjini Zanzibar wakitafakari kuhusu tukio la Padri Evarist Mushi kuuawa kwa kupigwa rirasi juzi mjini Zanzibar.
Mashuhuda waliozungumza na Mwandishi kwa nyakati tofauti walisema sababu zilizofanya padri wa awali, Ambrose Mkenda apigwe risasi siku ya mkesha wa Krismasi, mwaka jana ndizo zilizofanya na huyu auawe.
“Polisi wanaweza kujua zaidi kwa sababu tunadhani wanaendelea na uchunguzi kuhusu kupigwa risasi kwa padri Mkenda, watakuwa na fununu za kinachosababisha viongozi wa dini kushambuliwa,” kilisema chanzo chetu cha habari visiwani Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdalla Mwinyi (kushoto) akijumuika na wananchi kwenye uwanja wa hospitali ya Mnazi Mmoja kufuatia tukio hilo la kuhuzunisha.
Hata hivyo, kuna wengine walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa sababu za kupigwa risasi kwa viongozi hao wa kiroho ni itikadi za kidini ambazo uhasama wake unaongezeka kila kukicha hapa nchini.
“Ipo haja kwa serikali kuangalia hili kwani sisi watu wa dini nyingine hapa mjini (Zanzibar) tunaishi kwa wasiwasi,” alisema muumini mmoja wa Kanisa Katoliki.
Padri Cosmas Aman Shayo wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Joseph (kushoto) akijadiliana kuhusu tukio hilo na baadhi ya waumini kwenye uwanja wa hospitali ya Mnazi Mmoja  Zanzibar juzi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, ACP Aziz Mohamed alipopigiwa simu alisema atafutwe msaidizi wake ambaye hakupatikana kwa simu.
(Picha Zote na Martin Kabemba, Zanzibar)

MWILI WA MAMA NA WANAYE WATEKETEZWA KWA MOTO

Stori:  Dustan Shekidele, Morogoro
UNYAMA gani huu? Ni swali walilokuwa wakijiuliza wananchi baada ya kushuhudia mwili wa mama mmoja, Araga Hamza Stani  uliokuwa umechomwa moto pamoja na watoto wake wawili  Abdul (6) na Tarishi (1), Februari 10, mwaka huu katika Kijiji cha Kitete, wilayani Kilosa mkoani hapa.
Marehemu Araga Hamza Stani (kulia) enzi za uhai wake.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea wakati mama huyo na wanawe walipokuwa wamelala usiku ndipo watu wasiojulikana walipochoma moto nyumba ya nyasi waliyofikia kijijini hapo.
Shuhuda mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake  gazetini alisema tukio hilo limewashangaza wengi kwa sababu mama huyo na wanawe walifika kijijini hapo kwa ajili ya kuwasalimia ndugu zao wakitokea Dumila.
Mabaki ya mwili wa mama na watoto wake yakiwa yamebebwa kwenye pikipiki.
“Inavyoonekana kuna chuki kati ya marehemu na watu waliochoma nyumba lakini kinachoshangaza huyu mama hakai hapa, anaishi Dumila ambako anajishughulisha na na kazi ya ususi, hapa alikuja kusalimia tu,” alisema shuhuda huyo na kuhoji kosa la marehemu.
Mwandishi wetu alishuhudia miili ya mama na watoto wake iliyoteketea kwa moto ikifungwa kwenye mkeka na kusafirishwa kwa pikipiki ‘bodaboda’ kupelekwa Dumila kwa mazishi.
Polisi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na afisa mmoja wa ngazi ya juu amesema upelelezi umeshaanza

RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA KIONGOZI WA KANISA LA ORTHODOX POPE THEODOROS II IKULU JIJINI DAR





Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Kiongozi wa Kanisa la Orthodox Pope Theodoros II ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kiongozi huyo wa Kanisa la Orthodox yupo hapa nchini kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine atatembelea miradi mbalimbali inayoendeshwa na kanisa hilo hapa nchini ikiwemo Zahanati na shule ya msingi Iringa pamoja na Hospitali ambayo inaendelea kujengwa huko Bukoba Mkoani Kagera.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Kiongozi wa Kanisa la Orthodox Pope Theodoros II ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Kanisa la Orthodox Pope Theodoros II (wapili kushoto) mara baada ya kufanya mazungumzo na kiongozi huyo ikulu jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Askofu wa Mwanza na Bukoba Askofu Jeronymos. Nyuma ya Rais mwenye tai nyekundu ni mwenyekiti wa Hellenic society of Tanganyika Dimitris Mantheakis, na kulia ni askofu mkuu wa Dar es Salaam na mashariki askofu Dimistrious

(Picha na Freddy Maro-IKULU)

Sunday, February 17, 2013

TASWIRA ZA MKUTANO WA CCM KATIKA VIWANJA VYA PILE TEMEKE JIJINI DAR



Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akihutubia wananchi wa Wilaya ya Temeke na kuwahakikishia kuwa CCM itaisimamia serikali itekeleze ilani yake ya Uchaguzi kwa asilimia 100.

Juliana Shonza akihutubia wakazi wa Temeke juu ya maamuzi yake thabiti ya kujiunga na CCM.



Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Ndugu Sophia Mjema akiwapungia wananchi wa Temeke wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Pile, Temeke Mwisho.…






Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akihutubia wananchi wa Wilaya ya Temeke na kuwahakikishia kuwa CCM itaisimamia serikali itekeleze ilani yake ya Uchaguzi kwa asilimia 100.




Juliana Shonza akihutubia wakazi wa Temeke juu ya maamuzi yake thabiti ya kujiunga na CCM.




Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Ndugu Sophia Mjema akiwapungia wananchi wa Temeke wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Pile, Temeke Mwisho.





Wasanii wa kikundi cha TMK wakitoa burudani kwenye uwanja wa nyumbani wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Pile, Temeke, jana tarehe 16/2/2013.




Mtela Mwampamba akiwaeleza wananchi wa Temeke mapungufu makubwa ya kidemokrasia yaliyopo kwenye vyama vya upinzani na hivyo kumfanya yeye binafsi kuchukua uamuzi wa kujiunga na CCM.




Saumu Kisena akionyesha kitambulisho chake, Saumu amejiunga rasmi CCM baada ya kugundua chama alichokuwepo kinahubiri haki nje wakati ndani hamna haki kabisa.




Wananchi na wapenzi wa CCM kutoka kata ya Kilakala, Yombo kama walivyojitambulisha wakiwa katika mkutano huo.


Kikundi cha Hamasa cha CCM, Temeke kikihamasisha kwa aina yake wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Pile, Temeke jana.



Baadhi ya wananchi wakionekana kuelewa vizuri maneno ya viongozi wao.

                                              Picha na CCM BLOG

MASHABIKI WAMSHAMBULIA DIAMOND....WADAI AACHE "UMALAYA"


Katika kusherehekea Valentine’s Day, Diamond aliamua kupost picha inayomwonesha akiwa na mpenzi wake wa sasa Penny Mungilwa. 

Picha hiyo iliyowekewa effect na kufanya ionekane kama ya kuchora ina ujumbe usemao: @ ] diamondplatnumz #InstaSketch…..Happy Valentine everybody…#Live #Love #CelebrateLove #Eeer’day #EverydayIsAValentine.


Hata hivyo si wote waliopendezwa nayo. Mmoja wa followers wake, anayejiita ‘someuglymofo’ aliamua kumpa mbovu Diamond na kumwambia hana heshima kwa wanawake huku ujumbe wake akiuelekeza kwa Penny.

“Uuuuugh honestlly I’ve never seen anyone stoop so low like this….. out of all the people u could’ve bn wth u ended up with a trashymofo who has no respect for women he sleeps with them, abuses them and makes them look like sluts,I min cummoooooooooon…………….ts getting Penniel of all people Diamond it seems like u do not know when to stop, who to respect and honestly now I know u are one nasty mf,leave that girl elowne, ts not that hard to see she’s too good for you.(believe that,” aliandika.
770f70b8782b11e2b1f822000a1f9751_7
d44b95a4782b11e2b41b22000a1f9a15_7
“@vjpenny girl if ts true that you are preggers by that this low life of a man, ts onlly a matter of time before you realise he’s just using you just like any of his previous gf’s,(EVERY THING THIS GUY TOUCHES turns into dirt) make a wise choice while u still can dump his thilthy ass, he’s beneath you, that is not hard to see, look at what he did to@jokatem that girl was a Tanzanian sweetheart, people hated her and all was because of this disgusting piece of dirt, your decline is near God has a way of punishing evil bastards like you, get some respect for this beautiful Tanzanian.”

KUMBE GOLDIE ALIKUWA MKE WA MTU???...MUME WAKE AJITOKEZA NA USHAHIDI WA PICHA


Mwanaume wa kizungu aitwaye Andrew Harvey, anayedai kuwa amemuoa msanii wa muziki nchini Goldie Harvey aliyefariki juzi usiku amejitokeza na kupost picha za ndoa na mahaba wakiwa pamoja.

Andrew alishare picha hizo pia kwenye mtandao wa twitter na kuliambia gazeti la Nigeria Entertainment Today kuwa ana admin access za akaunti za mitandao ya kijamii ya marehemu Goldie.
goldie-his-9
goldie-hus3



goldie-hus-7-600x450
goldie-hus5-

goldie-hus-8-460x345

goldie-wed
goldie-wed-3
goldie-wed-4-460x345
Hii ni interview exclusive kati ya Andrew na gazeti hilo:

When did you wed her? And were you still married as at when she passed yesterday?

We wed in December 2005 and were very much married when she passed indeed I was talking to her on arrival in Lagos before the fateful event

I see you moved back to England. Do you have another family?

I work in Malaysia, we have a private home in UK, I do not have a second family

Also did you have kids together?
No kids, we were planning this year

There had been speculation for many years that she was married to an ‘oyinbo’ man. But no one could lay hands on anything. Why did you keep it a ‘secret’?
Our private life is nothing to do with work life, there has to be a balance

How did you hear of her death? I found out you last saw her in December?

I was talking to her on arrival in Lagos before the fateful event

How did you meet her? She must have been very young…

I met her at a friend’s leaving party and fell in love straight away, but had to work hard to persuade her I was genuine


So you will be planning to come here for burial rites…

Yes I have applied for visa and shall come next week

But how did you manage the Prezzo drama?
Prezzo was part of BBA game, just like in the movies, there was nothing to fear

But funny it dragged way beyond BBA
It dragged because the media dragged it, other wise it would have died naturally. Prezzo will say anything to get attention

Do you think he fell in love? And did you ever think Susan liked him for a minute…?

People fall in love and it’s not impossible to love more than one person, but there are different levels. She liked him initially, but began to despise him and distanced herself as he tried to use her she complained he was very manipulative

You have direct access to her password? The memories album was posted on her twitter. Or you requested for an admin to post?

I am an official admin. I don’t need any password but my own. It was authorised by Goldie

One last question: so much speculation on cause of death. I see from your facebook timeline that you’ve followed the reports. Have the doctors/family/label told you what the cause of death is?

An autopsy is being carried out and we will await results. The rest is speculation and hearsay

And did she have any medical condition?

She had no medical condition
Is it true she was in India recently?
She was in Malaysia, we spent Christmas together away from prying eyes
What will you miss most about her?

Everything, she was the most beautiful person I ever met, no moment was wasted. Sweet, intelligent, sexy and a magnificent cook!!!!

LULU USO KWA USO NA MAMA YAKE KANUMBA KWENYE KABURI LA KANUMBA


Pichani ni Elizabeth Michael/Lulu na Mama mzaz wa Marehemu Steven Kanumba (Face to Face Makaburini).

KAULI YA PREZZO KUHUSU KIFO CHA MCHUMBA WAKE GOLDIE



Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Prezzo ameandika jinsi anavyojisikia kufuatia kifo cha Goldie, msichana aliyekuwa amepanga kumchumbia.


God saw you were getting tired, and a cure was not meant to be. So he put his arms around you, and whispered come with me. With tearful eyes we watched you, as we saw you pass away.

 Although we love you deeply, we could not make you stay.Your golden heart stopped beating,hard working hands at rest. God broke our hearts to prove to us.He only takes the best.

Hizi ni tweets za baadhi ya mastaa wengine kufuatia msiba huo:

AY: Losing a loved one is very difficult for the people who live on,I mourn U till I join U, R.I.P Goldie .. You call me #SKIBOBOMASTER all the time.. Pole sana @AMB_Prezzo kuwa STRONG!!

MwanaFA: Doh… @GoldieHarvey …sasa ndio imenienea…kapumzike kwa amani mama…safari yetu wote,umetutangulia tu…

Mercy Johnson: Waje ooooooo,am so broken,remember we all did dinner before d wedding,awww waje,am hurt
Waje: Am so hurt,so hurt.RIP my dear friend GOLDIE
Kalu Ikeagwu: Goodnight Goldie. Go rest after all the day’s work.

Audu Maikori: Honest I do not even have the words to describe how distraught I am with the news of Goldie’s death! Gods will be done. We mourn her deeply
Seyi Law: Than you Lord for the Gift of Life…RIP Goldie Harvey, you’ll be greatly missed!

Lami Phillips: “The more i know;the less i understand” God keep your soul Goldie. Oluwa sanu fun wa.

Linda Ikeji: Finding it so difficult to sleep. Scared of closing my eyes. Young, vibrant people aren’t supposed to die so suddenly. RIP Goldie

Darey Art Alade: So sad hearing about Goldie…? big dreams gone just like that? Go well dear… Let’s celebrate her life #RIPGoldie

Stella Damasus: Rest in peace Goldie. We will miss you dearly. God grant your family the strength to bear the loss. It is well.

Terry Tha Rapman: God rest your soul, Goldie!
Banky W: My Goodness… i Just heard some terrible news.. RIP Goldie Harvey… wow. Lord bless her soul & have mercy on us all.

:-( 
  
Keitta Ossei Massai: Goldie! R.i.P! God be with you!

Uti Nwachukwu: Goldie I will celebrate you. Even in death.You were a kind woman that made a HUGE mark in africa. May God bless&accept ur soul IJN-Amen

PADRE WA KANISA KATOLIKI AUAWA KIKATILI KWA KUPIGWA RISASI ZANZIBAR

 

Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba Padre Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki Zanzibar ameuawa kikatili kwa kupigwa risasi tatu kichwani leo asubuhi. Padre Evarist alikuwa anakwenda kuongoza ibada takatifu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Teresia lililopo Mtoni Zanzibar. Marehemu alikuwa anakaribia kanisani majira ya saa 1.30 asubuhi na ameuawa mbele ya waumini wa kanisa lake. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN

Friday, February 15, 2013

MAGAZETI 16 YA LEO FEB 15

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.