Monday, September 23, 2013

MWILI WA PRIVATE HUGO BARNABAS WAAGWA LUGALO JIJINI DAR

  
Marehemu Privite Hugo Barnabas Mugo, enzi za uhai wake.
Jenerali Mwamunyange akisaini kitabu cha maombolezo.
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue akisaini kitabu cha maombolezo.
Balozi wa Tanzania nchini DRC akisaini kitabu cha maombolezo.
Askari akiwaonyesha ndugu wa marehemu sehemu ya kukaa.
Ndugu wa marehemu wakiwa wamekaa katika Viwanja vya Lugalo.
Mama wa marehemu (wa kwanza kushoto ) na dada wa marehemu wakienda kukaa sehemu waliyoandaliwa.
Hii ni sehemu maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kuweka mwili wa marehemu.
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Ndomba akisaini kitabu cha maombolezo kama anavyonekana.
Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Robert Mboma akikaribishwa katika viwanja hivyo.
Jenerali Mboma akisaini kitabu cha maombolezo.
Kikosi cha 94 Mwenge cha Brasibendi kikitumbuiza katika maombolezo hayo.
Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange (wa pili kutoka kushoto) akiwasili katika Viwanja  vya Lugalo leo saa asubuhi kwa ajili ya kuaga mwili wa askari wake.
  Jenerali Mwamunyange akisalimiana na maofisa wakuu.
Jenerali Mwamunyange akiteta jambo na Mnadhimu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali Ndomba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa akisaini kitabu cha maombolezo.
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Ombeni Sefue ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi akiwasili katika viwanja hivyo.
Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Mwamunyange akiteta jambo na Ombeni Sefue.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akisalimiana na baadhi ya viongozi alipowasili katika Viwanja vya Lugalo.
Mbowe akisalimiana na Jenerali Mwamunyange.
Wapiganaji wa JWTZ kama wanavyoonekana pichani wakiwa katika Viwanja vya Lugalo.
Mwili wa marehemu ukiwasili katika viwanja hivyo leo saa 5 asubuhi.
Ndugu wa marehemu wakiwa katika huzuni mkubwa.
Mwili wa Private Hugo ukipelekwa katika sehemu maalum kwa ajili ya kuagwa.
Mwili wa marehemu ukiwa tayari kwa kuagwa.
Katibu kiongozi akiongoza waombolezaji kwenda kuaga mwili wa Private Hugo.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa na Balozi wa Tanzania nchini  China na Luteni Jenerali Mstaafu Shimbo, nyuma yao ni Balozi wa Tanzania nchini DRC.
Jenerali Mwamunyange akiwapa mkono wa pole wafiwa.
Freeman Mbowe naye akiwapa mkono wa pole wafiwa.
Maafisa wakuu wa jeshi wakipita mbele ya mwili wa marehemu kutoa heshima za mwisho.
Ndugu wa marehemu wakiwa wameinamisha vichwa chini kwa huzuni.
Mmoja wa ndugu wa marehemu akilia kwa uchungu huku akisaidiwa na wanajeshi.
Jenerali Mwamunyange akisoma salamu za rambirambi za jeshi.
Mama na dada wa marehemu wakiwa katika hali ya huzuni.
Mwili wa marehemu ukipelekwa kwenye gari tayari kwa safari kuelekea mkoa wa Kilimanjoro kwa ajili ya mazishi.
Mama wa marehemu akisaidiwa na mwanajeshi kwenda kwenye gari tayari kwa safari.
Jenerali Mwamunyange akiondoka katika viwanja hivyo leo saa 12 .10 mchana.
MAJONZI, vilio na simanzi vilitawala leo katika Viwanja vya Jeshi, Lugalo jijini Dar es Salaam pale mwili wa Private Hugo Barnabas Mugo ulipowasili kwa ajili ya kuagwa.
Hugo alifariki dunia Septemba 18 mwaka huu baada ya kulipukiwa na bomu nchini DRC alipokuwa katika kikosi cha kulinda amani. Baada ya kulipukiwa na bomu alipelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.
Hafla ya kumuaga iliongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Sifuni Ombeni na JWTZ liliongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyage.
Katika  hotuba yake kwenye hafla hiyo, Jenerali Mwamunyange amesema kuwa kwa mara nyingine Tanzania imepata pigo kubwa kwa kumpoteza askari wake huyo shupavu.
Love to hear what you think!