Wednesday, September 25, 2013

KIJANA HUYU ANAOMBA MSAADA


Laurent John akionesha mguu wake unaomsumbua.
Kijana Laurent John mkazi wa Manzese, Darajani jijini Dar es Salaam, ameugua mguu wake wa kulia kwa muda mrefu na hivi sasa umevimba na unaelekea kuoza. Akiongea na mwandishi wetu, Laurent alidai ameteseka na tatizo hilo kwa muda mrefu sasa hali inayomfanya ashindwe kufanya shughuli zake baada ya kukosa fedha za matibabu. "Tatizo hili lilianza kama kipele kidogo na hivi sasa hali ya mguu huu imekuwa mbaya" Alisema Laurent. Kwa mtu yeyote atakayehitaji kumsaidia, Laurent anapatikana Manzese karibu na Msikiti wa Shidele jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA HARUNI SANCHAWA, GPL)
Love to hear what you think!