Saturday, August 24, 2013

AIBU YA UZINZI

Stori:Waandishi Wetu
KWELI duniani uaminifu kwa sasa ni sifuri! Hii ni aibu ya uzinzi! Jumatano iliyopita kwenye nyumba moja ya kulala wageni iliyopo Kurasini jijini Dar, Kennedy Shayo, mkazi wa eneo hilo, alimfumania ‘laivu’ swahiba wake, Sebastian Masangula akiwa kwenye harakati za ‘kubanjuka’ na mkewe, Fatuma Shayo, Risasi Jumamosi lina kila kitu.
Nimesha aibika Jamani
HABARI KAMILI
Kwa mujibu wa chanzo makini, kwa muda mrefu Masangula alikuwa akimtokea mke wa rafiki yake kwa meseji tam’tamu za simu huku akisisitiza kutaka kuvunja naye amri ya saba ya Mungu.
Huyu Mwanaume kila kitu nampatia,sijui amefuata kitu gani huku
Inadaiwa kuwa, mwanamke huyo alimuonya Masangula aache kumfutafuata lakini jamaa huyo akawa ‘sikio la kufa’ na kuendelea kumsumbua shemeji yake huyo akitaka apewe penzi japo kiduchu.
Ninaumbuka!
MTEGO WA KUMNASA MASANGULA WAANDALIWA
Baada ya Masangula kumsumbua shemeji yake kwa muda mrefu, mwanamke huyo alimuweka wazi mumewe ambaye alishtuka kupita maelezo ndipo wakaandaa mtego wa fumanizi kwa kuwashirikisha mapaparazi wetu wa kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’.
Yani huyu baba amenisumbua muda mrefu sana akinitaka
Mtego huo ulianza kutegwa mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya Masangula kumuomba shemeji yake huyo wakutane kwenye gesti hiyo.
Siku ya tukio wawili hao walifika eneo hilo lakini Masangula kama machale yalimcheza na kuchoropoka kwenye fumanizi kwa kuomba udhuru huku akimwambia shemejiye kwamba waivunje amri ya saba siku nyingine.

Mungu wangu aibu gani hii mimi? Nisameheni Jamani
LA KUVUNDA HALINA UBANI
Kama methali ya wahenga isemavyo ‘la kuvunda halina ubani’, ndivyo ilivyokuwa kwa Masangula kwani licha ya machale kumcheza siku ya kwanza na kuchoropoka, wiki iliyopita aliendelea kuomba penzi kwa shemejiye ndipo mtego ukapangwa tena na mzee mzima safari hii alinaswa laivu kitandani akimtolea udenda shemeji yake huku akiwa na kufuli tu. Shemeji mtu naye alifanya ‘magilini’ kama anataka kuvua nguo zake.
Mwanamke huyo kabla ya kuvua alimtonya mumewe aliyekuwa nje na mapaparazi kwamba, jamaa yuko kama alivyozaliwa, ndipo kikosi kazi kikavamia kwenye chumba namba nne ndani ya gesti hiyo na kumnasa Masangula.

MASANGULA ASHIKWA UGONI
Ndani ya chumba, mwenye mke aligongana uso kwa uso na Masangula aliyekuwa tayari kwa mechi.  Tukio hilo lilimfanya mgoni huyo achanganyikiwe na kushika tama kwa aibu huku akiomba msamaha kwa maneno mbalimbali ya huruma.

UMATI WAFURIKA
Dakika moja mbele, umati mtaani ulifurika kwenye gesti hiyo kila mmoja akitaka kuwaona waliofumaniwa.

MKE WA MASANGULA AITWA AONE AIBU YA MUMEWE
Baadhi ya wapambe walimpigia simu mke wa Masangula (mama Gire) afike eneo la tukio kushuhudia aibu ya mumewe lakini simu ya mama Gire ikawa haipatikani.
Wapambe hao waliamua kukodi Bajaj kumfuata kisha kumpeleka eneo la tukio.
Baada ya kufika, mama Gire alipigwa butwaa kumwona mumewe alivyonaswa.
“Masikini ya Mungu baba Gire, hivi umekosa nini nyumbani mume wangu? Hii aibu gani mume wangu, umenidhalilisha sana mtaani, huyo Shayo si unasemaga ni rafiki yako siku zote? Sasa leo iweje utake kumsaliti?”
Licha ya kuulizwa maswali na mkewe lakini mgoni huyo hakujibu chochote zaidi ya kujikunyata na kuwapigia magoti mkewe na rafiki aliyetaka kumsaliti kwa mkewe.

MAMA SHAYO ALONGA
Wakati mke wa Masangula akijutia aibu ya mumewe, Fatuma alianza kumwelezea  Masangula jinsi alivyoanza kumfukuzia kwa muda mrefu.
“Mumeo kwa muda mrefu alikuwa akinitongoza, najua lengo lake alikuwa akitaka anidhalilishe lakini kakuta mimi siyo mtu wa kihivyo,” alisema.
Naye mume wa Fatuma, akizungumza na mapaparazi wetu alisema amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na swahiba wake huyo ambaye walikuwa kama ndugu.
“Mke wangu alivyonieleza mara ya kwanza sikumuamini, nikajua ni mambo ya wanawake, anataka kunigombanisha na rafiki yangu, lakini baada ya kunionesha ujumbe aliokuwa akitumiwa na ni namba ya rafiki yangu nilipigwa butwaa,” alisema Shayo huku akionekana mwenye jazba.
Hadi mapaparazi wetu wanaondoka eneo la tukio, Shayo alikuwa katika harakati za kumfikisha mgoni wake kwenye vyombo vya dola.
HABARI IMEANDIKWA NA RICHARD BUKOS, ISSA MNALLY NA IMELDA MTEMA.Love to hear what you think!