Saturday, June 8, 2013

SEND OFF YA FLORA MVUNGI YAPIGWA UMBEYA

Stori:Imelda Mtema
SEND OFF ya ua zuri kwenye soko la filamu Bongo, Flora Mvungi iliyofanyika Jumanne iliyopita Msasani Beach, Mikocheni jijini Dar imepigwa umbea kuwa ni bosheni kwani hata ndoa yake na Hamis Ramadhan ‘H. Baba’ haitadumu kutokana na tabia ya wasanii kutodumu kwenye ndoa.
Mmoja wa wasanii waliohudhuria sherehe hiyo na kuomba hifadhi ya jina, amepenyeza habari kuwa ndoa ya mastaa hao inayotarajiwa kufungwa Jumamosi hii (leo) haitadumu kwani mara nyingi wasanii wanakuwa na tabia za kutotulia hivyo wanaipa mwaka mmoja, itavunjika.
“Yaani hiyo ndoa mimi nawaambia nawapa mwaka mmoja tu mtaniambia kama kutakuwa na ndoa tena, wasanii ni wasanii tu hata iweje. Tatizo lao wanaleta maisha ya kuigiza hadi kwenye filamu.
“Tazama ndoa ya Uwoya ilivyokuwa ya gharama, mbwembwe nyingi lakini mwisho imekuja kuparanganyika huku kila mmoja akimtafuta mwenzake uchawi,” alisema msanii huyo ambaye anaonesha ‘kuwajua’ vizuri wanandoa hao.
Siku ya send off, Flora alipotinga ukumbini na kubadilisha mavazi zaidi ya matatu, ilidaiwa kuwa ni ufahari na mara nyingi huwa ndoa za namna hiyo kwa mujibu wa msanii huyo hazidumu.
“Ni mbwembwe tu zisizokuwa na msingi wowote, Flora na H. Baba tunawajua vizuri, kama hamuamini subirini mtaona, ikizidi mwaka mmoja ni bahati,” alisema.
Hata hivyo, Flora baada ya kumaliza sherehe hiyo alidai kuwa anamuomba Mungu ndoa yao idumu milele na milele ili kuwakata vilimi wambeya wote wasioitakia mema ndoa yao.
“Tunamuomba Mungu ndoa yetu idumu vizazi na vizazi na hao wanaochongachonga kila kukicha wabaki midomo wazi sisi maisha yanaendelea,” alisema Flora.
Sherehe hiyo ya send off ilihudhuriwa na mastaa kadhaa wa Bongo Movies akiwemo Jacqueline Wolper, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’, Isabela Mpanda na Luteni Kalama.Love to hear what you think!