Thursday, April 11, 2013

NAIBU WAZIRI WA ELIMU ATANGAZA KUWASHITAKI WANAODAI KUWA "AMEGUSHI VYETI" NA ANATUMIA MAJINA YA WATU

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amesema atawafikisha mahakamani watu wanaodai kuwa ameghushi vyeti vya elimu ya sekondari.  Mulugo alisema amechoshwa na kashfa hizo zinazosambazwa na baadhi ya watu atawafikisha mahakamani endapo wataendelea kumdhalilisha. 
Mulugo alitoa kauli hiyo alipofungua mkutano wa mwaka wa Umoja wa Wamiliki wa Shule za Sekondari na Vyuo Binafsi Tanzania (TAMONGSCO0) jijini Mbeya.

“Wanasema eti nimeghushi vyeti, mara ooh sijui natumia jina la mtu. Nimechoshwa na maneno haya… ni kweli nimerudia darasa kama walivyorudia watu wengine, kwa nini iwe tatizo kwangu. Hata hapa tulipo wapo wengi tu waliorudia darasa.

“Kama kweli ningekuwa nimeghushi vyeti hivi leo ningekuwa naibu waziri wa elimu? Sasa nimechoshwa, nitawachukulia hatua watu hawa, siwezi kusema ni lini nitafanya hivyo ila nitakapoamua nitaanza,”alisema.

Kwa miezi kadhaa sasa Mulugo amekuwa akidaiwa kughushi vyeti na kutumia jina la mtu ili kufikia kiwango cha elimu alichonacho madai ambayo alisema yanamchafulia jina katika jamii.

Kuhusu suala la matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana, Mulugo alisema matokeo hayo mabaya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na mmomonyoko wa maadili miongoni mwa wanafunzi.

Naye Ruth Mnkeni kutoka Dar es Salaam anaripoti kuwa Mlugo amezindua tovuti ya elimu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ijulikanayo kama Shule Direct.

Muluigo alisema kuzinduliwa kwa tovuti hiyo kutawafanya wanafunzi kupata maarifa mengi ya vitabu mbalimbali na kuinua kiwango cha elimu nchini



Love to hear what you think!