Thursday, April 11, 2013

MTOTO AUAWA KIKATILI JIJINI MBEYA KWA KUNYOFOLEWA KICHWA NA MGUU MMOJA

  IMANI za kishirikina zimezidi kukitisa Kijiji cha Isange na Kata ya Isange baada ya matukio ya kupotea na kuawa kwa Watoto kutokea mara kwa mara ambapo Marehemu hukutwa wakiwa na mapungufu ya viungo ikiwemo Kichwa.


Katika tukio la hivi karibuni Mtoto mmoja aliyejulikana kwa Jina la Lista Sebule (8) Mwanafunzi wa Darasa la Saba katika  Shule ya Msingi Mpombo  iliyo katika Kata ya Isange Halmashauri ya Busokelo Wilaya ya Rungwe Mkoani hapa  alipotea katika mazingira ya kutatanisha na kukutwa baada ya Siku 9 akiwa amekufa.
  
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Mama mzazi wa Marehemu Christina Sakalile alisema binti yake alipotea majira ya saa tisa jioni Machi 31, Mwaka huu baada ya kutumwa kupeleka simu kibandani ili kuchaji lakini hakurudi hadi Saa Kumi na Mbili jioni hali iliyozua wasiwasi na kuanza kumtafuta bila mafanikio.

Alisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa Kijijini ambapo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Isange Daudi Nsyani ambaye baada ya kupewa taarifa hizo pia aliwataarifu viongozi wa Kata akiwemo Diwani wa Kata ya Isange Elias Mwasandele na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo Brayson Nguro ambaye aliitisha Mkutano wa wananchi.
  
Mtendaji huyo aliwaambia wananchi hao kushirikiana ili Mtoto apatikane hali ambayoiliitikiwa na wananchi ambao walitaka Mtoto apatikane aidha akiwa mzima ama Mfu ambapo juhudi za kumtafuta zilianza na hatimaye kumpata Aprili 8, Mwaka huu akiwa amekufa huku akiwa hana baadhi ya Viungo.
  
Mashuhuda wa tukio hilo walisema Mwili wa Marehemu ulipatikana ukiwa pembezoni ya Mto Nkalisi uliopo Kijijini hapo ukiwa umenyofolewa baadhi ya viungo kama Kichwa na Miguu ambapo mguu mmoja ulipatikana baada ya Mbwa kukutwa akiwa ameshika na kuudondosha baada ya kukutana na watu hali iliyowalazimu watu hao kumfutilia Mbwa huyo aliyeongoza hadi Mwili wa Marehemu ulipokuwepo na kuwakuta Mbwa wengine wawili wakiwa pembezoni.


Baada ya kupatikana kwa mwili huo Taarifa ilipelekwa Polisi ambao walifika katika eneo la tukio na kuupima kisha kuwakabidhi ndugu kwa ajili ya mazishi ambapo  watu wawili walikamatwa kuhusika na tukio hilo baada ya kupigiwa kura za siri na wananchi na kukutwa na kura nyingi ambapo wengine wanne waliachiwa kutokana na kutokuwa na kura nyingi.
  
Kutokana na hali hiyo Ofisa Mtendaji wa kata hiyo alisema mfululizo wa vitendo hivyo unatokana na kutokuwa na Vituo vya Polisi ambapo Halmashauri ya Busokelo inakituo kimoja kilichopo katika Mji wa Lwangwa mahali ambapo ni mbali sana kutokana na gharama kuwa kubwa.


Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Elias Mwandele alisema wananchi waache kutembea usiku ambapo aliongeza kuwa Vilabu vya Pombe vifungwa saa mbili usiku huku akiwataka Wazazi kutowapeleka watoto kwenye Shughuli za Machungo ambapo wameweka ulinzi wa Sungusungu ili kudhibiti hali hiyo.

SAMAHANI KWA PICHA HII HATUJAIONYESHA VIZURI SABABU MWILI WA MTOTO LISTA UMEHARIBIKA VIBAYA HIVYO TUMEONA SI VYEMA KUUONYESHA WOTE
MARA TU BAADA YA POLISI KUUTOA MWILI PORINI NA KUUCHUNGUZA WALIWAKABIDHI WAZAZI  ILI WAENDELEE NA TARATIBU ZA MAZISHI YA MTOTO LISTA
MGUU WA MAREHEMU LISTA
MWANA USALAMA AKIWA AMEUSHIKA MGUU WA MTOTO LISTA MARA TU BAADA YA KUUPATA MWILI WAKE PORINI NA KUKUTA HANA BAADHI YA VIUNGO VYAKE VYA MWILI
UMATI MKUBWA ULIOHUDHURIA MAZISHI YA MTOTO LISTA


Habari picha na Mbeya yetu



Love to hear what you think!