Sunday, December 9, 2012

Sintah Asita Kuanika Hadharani Mali Anazomiliki

MSANII wa filamu bongo ambaye pia ni mtangazaji Christine John ‘Sintah’, ameuambia mtandao wa DarTalk, kuwa hawezi kuanika mali zake hadharani na watu wakazijua.

Wapo baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wakitangaza mali zao, ikiwemo ulimiki wa nyumba, magari au makampuni, ambapo kwa mwanadada huyo imekuwa tofauti kwa madai kuwa bado hajafikia hatua ya kuziweka mali zake hadharani.

Alisema kuwa hawezi kusema ana mali nyingi au anamiliki vitu vingi vinavyomuigiziapesa bali vipaji vyake ndiyo utajili wake kwani mbali na filamu pia ni MC, mfanyabiashara, Balozi, pia ni mtangazaji lakini ishu nyingine anazofanya alidai ni siri yake.

“We suala la kuanika mali bongo hukawii kuambiwa fisadi na kama huna kabisa utaambiwa umefulia sitaki mie, lakini kwa wanaojua maisha yangu wanajua ila kwa mashabiki wangu kweli napenda kuwambia maisha yangu ni ya kawaida” aliongeza.


Love to hear what you think!