Tuesday, December 4, 2012

MWANAFUNZI AFARIKI DUNIA KWA KUANGUKIWA NA UKUTA AKITAKA KUHUDHURIA TAMASHA LA MTIKISIKO IRINGA

Sehemu ya ukuta iliyobomoka na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja.
Wasamaria wema wakijaribu kumwokoa kijana aliyeangukiwa na ukuta kwa kufukua kifusi kwa mikono.…
Sehemu ya ukuta iliyobomoka na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja.
Wasamaria wema wakijaribu kumwokoa kijana aliyeangukiwa na ukuta kwa kufukua kifusi kwa mikono.
Sehemu ya ukuta uliobomoka.
MWANAFUNZI wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Kwakilosa katika Manispaa ya Iringa Daniel Yona (15) amefariki dunia baada ya kuaungukiwa na ukuta wa uwanja wa Samora wakati akijaribu kupita mlango wa panya ili kwenda kushuhudia tamasha la Mtikisiko 2012.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 2 mwaka huu wakati wapenda burudani katika mkoa wa Iringa walipofika katika uwanja huo kushuhudia onyesho kubwa la Mtikisiko 2012 ambalo lilikuwa limepambwa na wasanii mbali mbali wakiongozwa na mkongwe Juma Nature na Profesa J.
Wakielezea kilichomkuta mwanafunzi huyo baada ya mashuhuda walisema kuwa mwanafunzi huyo na wenzake waliacha kupita katika mlango wa kawaida kwa kulipia kiingilio halali kilichowekwa na badala yake aliamua kupita gizani na kupanda ukuta huo wa uwanja wa Samora ili kuweza kuingia ndani ya uwanja huo kuona tamasha la Mtikisiko.
Hata hivyo mmoja kati ya mashuhuda ambae hakupenda kutajwa jina lake hapa alisema kuwa kabla ya mwanafunzi huyo kupanda ukuta huo kuna vijana kama 20 ambao walifanikiwa kupita eneo hilo bila kulipa kiingilio na baada ya kufanikiwa kupita walianza kupigiana simu huku baadhi ya vijana wa kitanzini wakiwatoza vijana hao wanaoruka ukuta kiingilia cha shilingi 1000 hadi shilingi 500 .
"Ujue hapa vijana wa kihuni kutoka Kitanzini walikuwa wamejipanga hapa na kufanya ufisadi wa kuwatoza watu kiingilio bila wahusika wa Tamasha hilo kujua kinachoendelea .....hivyo hata huyo mwanafunzi alikuwa ni mmoja kati ya wavamizi wa Tamasha hilo kwa kupita njia ya panya ili kuingia ndani ya uwanja huo"
Pia alisema ukuta huo ulionyesha kuzidiwa nguvu kutokana na ubovu wa ukuta wenyewe kuwa ni mbovu na ulikuwa umeungwa kienyeji katika eneo hilo.
Aidha alisema baada ya vijana zaidi ya watano kupanda eneo hilo la ukuta ambalo lipo upande wa kushoto mwa uwanja huo wa uwanja ukuta huo ulionyesha kuyumba na kupelekea vijana wengine kuruka na kumwacha mwanafunzi huyo ambae tayari alikuwa ameingiza mguu mmoja ndani ya uwanja na mguu wa pili ulikuwa nje. 
Alisema baada ya ukuta huo kuanguka na kumfunika walifanikiwa kumwokoa akiwa hai na kumkimbiza Hospitali ya mkoa wa Iringa ambako asubuhi ya siku ya pili ya Desemba 2 majira ya saa 5 asubuhi alifariki dunia.
Hata hivyo askari polisi waliokuwepo eneo hilo la tukio walimthibitishia mwandishi wa mtandao huu kuwa ni kweli kijana huyo amefariki dunia japo wao si wasemaji wa jeshi la polisi na kudai kuwa chanzo ni kijana huyo mwenyewe kutaka kupita mlango wa panya na kuacha kupita mlangoni ambako watu wote walikuwa wakipita bila kupata matatizo yoyote.
Hata hivyo uchunguzi wa mtandao huu unaonyesha kuwa kifo cha mwanafunzi huyo kimesababishwa na mwanafunzi mwenyewe kutokana na kutaka kupita njia ya panya na kuacha mlango kwani iwapo angetumia njia sahihi kuingia uwanjani yawezekana kifo kisingeweza kutokea.




Love to hear what you think!