Thursday, July 26, 2012

NABII FLORA ATIBU UKIMWI WAUMINI WATOA USHAHIDI



Na Haruni Sanchawa
WAUMINI wa dini mbalimbali Jumapili iliyopita walijitokeza mbele ya Kanisa la Maombezi lililopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam kumshukuru na kutoa ushuhuda wao wa kupona Ukimwi.
Hali hiyo ambayo ilizua msisimko mkubwa kanisani hapo, ilishuhudiwa na mwandishi wetu ambapo watu zaidi ya kumi walionesha vyeti vyao baada ya kupimwa katika hospitali tofauti na kuthibitishwa kupona maradhi hayo.
Umati uliokuwepo kanisani hapo ulikuwa ukipiga vigelegele kuthibitisha kuwa walikuwa wamepona... ...baada ya kupata maombezi ya Nabii Flora.
Mwandishi wetu alipata nafasi ya kufanya mahojiano na baadhi ya waumini wa kanisa hilo ambao wengi wao waliyasifu maombezi ya Nabii Flora na kusema kuwa ni mazito na yenye kuponya magonjwa sugu.
“Pia yanasaidia kurudisha ndugu waliopotea na kuwarejesha pamoja watu walioachana kwa muda mrefu,” alisema muumini mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Merry Lwaluu.

BAADHI YA WALIOTOA USHUHUDA
Mwandishi wetu alifanikiwa kuwahoji baadhi ya waumini waliotoa ushuhuda wa kupona Ukimwi.
Asha Musa: Nilijigundua kuwa na Ukimwi miaka nane iliyopita, nilikuwa natumia vidonge lakini havikunisaidia lakini tangu nilipofika katika kanisa hili, mambo yangu yanakwenda vizuri sana. Namshukuru Mungu.
Navon Paskamoshilo: Mimi naishi Goba jijini Dar es Salaam, nilikuwa nimeathirika kwa muda mrefu na nilishakata tamaa ya kuendelea na maisha baada ya mwaka 2000 kupimwa na kugundulika kuwa nimeathirika.
Ndugu na jamaa zangu walinitenga lakini muumini mmoja wa kanisa hili akanishawishi kuja hapa, leo hii nimepona, nimerudia kupima mara kadhaa na nimegundulika niko fiti. Namshukuru sana mchungaji (Nabii Flora) na Mungu kwa kuniponya.”
Jane Mpangala: Nilipopima na kugundulika kuwa nimeathirika, shughuli zangu zilisimama kwa muda mrefu kwani sikuwa na nguvu ya kuzifanya. Nabii Flora amefanya miujiza yake sasa nimeanza kusafiri kuelekea sehemu mbalimbali kwa ajili ya shughuli zangu. Nimepona




Love to hear what you think!