Licha ya paparazi wetu kumdodosa aseme habari hizo, alikataa na kusema itakuwa ni sapraiz.
“Nina furaha sana kwa sababu nimerudi salama kutoka Dubai nilikokuwa nalazimishwa kufanya kazi za ndani nikakataa, ukweli watoto wangu wamefurahi sana kwa sababu nimerudi nikiwa na afya njema.
“Nina furaha sana kwa sababu nimerudi salama kutoka Dubai nilikokuwa nalazimishwa kufanya kazi za ndani nikakataa, ukweli watoto wangu wamefurahi sana kwa sababu nimerudi nikiwa na afya njema.
“Niko fiti nimeachana na madawa ya kulevya sasa hivi nimerudi rasmi
kwenye kazi yangu ya unenguaji, nitakutafuta siku nikupe habari kubwa
ambayo sijawahi kuzungumza sehemu yoyote yaani itakuwa ni nzuri na
utatoa magazeti matatu,” alisema Aisha ambapo Desemba 17, mwaka huu
alifariki dunia kabla ya kutimiza ahadi hiyo kwa mwandishi wetu.Aisha
aliyeacha watoto wawili wa kiume na wa kike, alitarajiwa kuzikwa jana
nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar.