Waziri wa uchukuzi Dkt. Harrisoni Mwakyembe amebaini wizi wa mafuta katika boya la mafuta mjimwema na kuagiza maskari wa usimamizi wa bandari Tanzania kuwakilisha majina ya wahusika ndani ya siku mbili.
Mwakyembe ameyasema hayo wakati akizungumza na wafanyakazi wa mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania (TPA) na kulaani kitendo cha baadhi ya watu kutoboa bomba hilo na kuunganishia mabomba yao madogo na kuyafungia kwenye maputo yenye uwezo wa kubeba mafuta kati ya lita 16-18 kinyume cha sheria na kukiita kitendo hicho ni kuhujumu uchumi wa nchi ambapo ameishutumu kampani ya ulinzi ya tipa kuhusika na kitendo hicho na kuwataka kumpa picha za wafanyakazi wote waliokuwa kitengo cha ulinzi na kama hawatafanya hivyo kampuni hiyo italipishwa fidia.
Naye kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania Mhandisi Madeni Kipande wakati akijibu mapendekezo yaliyotolewa na waziri mwakyembe kuhusu wafanyakazi wa mamalaka hiyo amesema kuwa wafanyakazi waliokuwa wameajiriwa kama vibarua watapewa ajira za kudumu na kubainisha kuongezewa posho wafanyakazi hao kutoka laki moja awali na kufikia laki mbili pamoja na laki moja na nusu kama ghrama za chakula
-ITV