Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina moja
la Damian, mkazi wa Ukonga Mazizini jijini Dar es Salaam, amekutwa
hajitambui kutokana na hali iliyonekana ni ya kupigwa. Kwa mujibu wa
wananchi wa eneo hilo, kijana huyo anayedaiwa kupigwa na watu
wasiojulikana, ametambuliwa kuwa ni mkazi wa hapo na pia
anajishughulisha na biashara ndondogo katika soko la Karume, wilaya ya
Ilala jijini Dar es Salaam.