NISHA ambaye ni msanii wa filamu hapa nchini ameamua kuvunja ukimya na kusimulia kinagaubaga juu ya ajali iliyomtokea majuzi wakati akitoka location na kusema kuwa kabla ya kupata ajali alikua mzima kabisa na aliweza kufanya kazi zake zote locationa mpaka mida ya saa saba za usiku...
"Wakati anarudi nyumbani anasema alifika sehemu akajisikia kizunguzungu na kuona kiza baada ya hapo ndipo aliposhtukia akiingia porina na gari kupinduka na kupata ajali hiyo".....NISHA
Nsha anadai kuwa hataki kulihusisha tukio hilo na kitu chochote bali ni mipango ya mwenyezi mungu na amesema kwa sasa hali yake si nzuri sana hivyo anaomba watanzania wamuombee ili aweze kupona haraka na aweze kurejea katika shughuli zake kama kawaida
DIAMOND NAYE ANUSURIKA KUFA.....
Juzi Diamond akiwa na gari lake alipata ajali ambayo ilisababisha sehemu ya mbele kuharibika. Kwa mujibu wa meneja wake, Raqey Mohamed wa I-View Media ajali hiyo ilisababishwa na mwendesha pikipiki.