Tuesday, February 19, 2013

MWILI WA MAMA NA WANAYE WATEKETEZWA KWA MOTO

Stori:  Dustan Shekidele, Morogoro
UNYAMA gani huu? Ni swali walilokuwa wakijiuliza wananchi baada ya kushuhudia mwili wa mama mmoja, Araga Hamza Stani  uliokuwa umechomwa moto pamoja na watoto wake wawili  Abdul (6) na Tarishi (1), Februari 10, mwaka huu katika Kijiji cha Kitete, wilayani Kilosa mkoani hapa.
Marehemu Araga Hamza Stani (kulia) enzi za uhai wake.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea wakati mama huyo na wanawe walipokuwa wamelala usiku ndipo watu wasiojulikana walipochoma moto nyumba ya nyasi waliyofikia kijijini hapo.
Shuhuda mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake  gazetini alisema tukio hilo limewashangaza wengi kwa sababu mama huyo na wanawe walifika kijijini hapo kwa ajili ya kuwasalimia ndugu zao wakitokea Dumila.
Mabaki ya mwili wa mama na watoto wake yakiwa yamebebwa kwenye pikipiki.
“Inavyoonekana kuna chuki kati ya marehemu na watu waliochoma nyumba lakini kinachoshangaza huyu mama hakai hapa, anaishi Dumila ambako anajishughulisha na na kazi ya ususi, hapa alikuja kusalimia tu,” alisema shuhuda huyo na kuhoji kosa la marehemu.
Mwandishi wetu alishuhudia miili ya mama na watoto wake iliyoteketea kwa moto ikifungwa kwenye mkeka na kusafirishwa kwa pikipiki ‘bodaboda’ kupelekwa Dumila kwa mazishi.
Polisi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na afisa mmoja wa ngazi ya juu amesema upelelezi umeshaanza


Love to hear what you think!