Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Kiongozi wa Kanisa la Orthodox Pope Theodoros II ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kiongozi huyo wa Kanisa la Orthodox yupo hapa nchini kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine atatembelea miradi mbalimbali inayoendeshwa na kanisa hilo hapa nchini ikiwemo Zahanati na shule ya msingi Iringa pamoja na Hospitali ambayo inaendelea kujengwa huko Bukoba Mkoani Kagera.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Kiongozi wa Kanisa la Orthodox Pope Theodoros II ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Kanisa la Orthodox Pope Theodoros II (wapili kushoto) mara baada ya kufanya mazungumzo na kiongozi huyo ikulu jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Askofu wa Mwanza na Bukoba Askofu Jeronymos. Nyuma ya Rais mwenye tai nyekundu ni mwenyekiti wa Hellenic society of Tanganyika Dimitris Mantheakis, na kulia ni askofu mkuu wa Dar es Salaam na mashariki askofu Dimistrious
(Picha na Freddy Maro-IKULU)