Friday, February 15, 2013

BREAKING NEWS: GOLDIE AMBAYE NI MCHUMBA WA PREZZO AFARIKI DUNIA



Yule Mwanadada kutoka Nigeria aliyeshiriki katika Big Brother Africa Star game na baadaye kuanza mahusiano ya kimapenzi na rapper wa Kenya Prezzo, amefariki dunia.
Msanii huyo aliyeimba nyimbo ya Skibobo, akiwa amemshirikisha AY, aliaga dunia mapema jana, muda mfupi tu baada ya kurudi akitokea Marekani alipokua ameenda kushuhudia tuzo za Grammys.

Goldie, inasemekana aliugua ghafla na hapo hapo kufariki. Meneja wa msanii huyo alidhihirisha habari hizi kupitia account ya twitter ya Goldie kwa kusema; 

Tumejaribu kupata mawasiliano na Prezzo atoe tamko, lakini hatujafanikiwa.

Tunatoa pole kwa Prezzo, familia ya Goldie Harvey, wasanii wenzake pamoja na fans wa mwanadada huyu.



Love to hear what you think!